Deuteronomy 26:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utamwendea kuhani anayehudumu wakati huo, na kumwambia, ‘Leo ninakiri mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, kuwa nimeingia katika nchi aliyowaapia wazee wetu kuwa atatupa.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na umwambie kuhani atakayekuwepo wakati huo, “Ninatangaza leo kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwamba nimekuja katika nchi ambayo Mwenyezi Mungu aliwaapia baba zetu kwamba atatupa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ukamwendee kuhani atakayekuwapo siku zile, ukamwambie, Ninakiri leo kwa Bwana, Mungu wako, ya kuwa nimeingia katika nchi Bwana aliyowaapia baba zetu ya kwamba atatupa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utamwendea kuhani anayehudumu wakati huo, na kumwambia, ‘Leo ninakiri mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, kuwa nimeingia katika nchi aliyowaapia wazee wetu kuwa atatupa.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na umwambie kuhani atakayekuwapo kwa wakati huo, “Ninatangaza leo kwa BWANA Mungu wako kwamba nimekuja katika nchi ambayo BWANA aliwaapia baba zetu kwamba atatupa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na umwambie kuhani atakayekuwepo kwa wakati huo, “Ninatangaza leo kwa bwana Mwenyezi Mungu wako kwamba nimekuja katika nchi ambayo bwana aliwaapia baba zetu kwamba atatupa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ukamwendee kuhani atakayekuwapo siku zile, ukamwambie, Ninakiri leo kwa BWANA, Mungu wako, ya kuwa nimeingia katika nchi BWANA aliyowaapia baba zetu ya kwamba atatupa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utamwendea kuhani anayehudumu wakati huo, na kumwambia, ‘Leo ninakiri mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, kuwa nimeingia katika nchi aliyowaapia wazee wetu kuwa atatupa.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Utakapofika umwendee mtambikaji atakayekuwapo siku hizo, umwambie: Leo hivi ninamshuhudia Bwana Mungu wako, ya kama nimeingia katika hiyo nchi, Bwana aliyowaapia baba zetu kutupa sisi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ukamwendee kuhani atakayekuwapo siku zile, ukamwambie, Ninakiri leo kwa BWANA, Mungu wako, ya kuwa nimeingia katika nchi BWANA aliyowaapia baba zetu ya kwamba atatupa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utamwendea kuhani anayetumika wakati huo, na kumwambia: ‘Leo ninashuhudia mbele ya Yawe, Mungu wangu, kwamba nimeingia katika inchi aliyowaapia wazee wetu kwamba atatupatia’.