Deuteronomy 26:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
utatamka maneno haya mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako: ‘Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyetangatanga huko na huko, kisha akashuka kwenda Misri akaishi huko kama mgeni. Yeye na jamaa yake walikuwa watu wachache tu walipokuwa huko, lakini wakawa taifa kubwa lenye nguvu na watu wengi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha utatangaza mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wako: “Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyekuwa anatangatanga, akaenda Misri pamoja na watu wachache, akaishi huko hadi akawa taifa kubwa, lenye nguvu na watu wengi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe ujibu, ukaseme mbele za Bwana, Mungu wako, Baba yangu alikuwa Mwarami karibu na kupotea, akashuka Misri, akakaa huko ugenini, nao ni wachache hesabu yao; akawa taifa kubwa huko, yenye nguvu na watu wengi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
utatamka maneno haya mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako: ‘Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyetangatanga huko na huko, kisha akashuka kwenda Misri akaishi huko kama mgeni. Yeye na jamaa yake walikuwa watu wachache tu walipokuwa huko, lakini wakawa taifa kubwa lenye nguvu na watu wengi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha utatangaza mbele za BWANA Mungu wako: “Baba yangu alikuwa Mwarami aliyekuwa anatangatanga, akaenda Misri pamoja na watu wachache akaishi huko akawa taifa kubwa, lenye nguvu na watu wengi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha utatangaza mbele za bwana Mwenyezi Mungu wako: “Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyekuwa anatangatanga, akaenda Misri pamoja na watu wachache, akaishi huko hadi akawa taifa kubwa, lenye nguvu na watu wengi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe ujibu, ukaseme mbele za BWANA, Mungu wako, Baba yangu alikuwa Mwarami karibu na kupotea, akashuka Misri, akakaa huko ugenini, nao ni wachache hesabu yao; akawa taifa kubwa huko, yenye nguvu na watu wengi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
utatamka maneno haya mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako: ‘Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyetangatanga huko na huko, kisha akashuka kwenda Misri akaishi huko kama mgeni. Yeye na jamaa yake walikuwa watu wachache tu walipokuwa huko, lakini wakawa taifa kubwa lenye nguvu na watu wengi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha uanze kusema mbele ya Bwana Mungu wako kwamba: Baba yangu alikuwa Mshami mwenye kutangatanga, akashuka Misri, akakaa huko ugenini pamoja na watu wachache, akapata kuwa huko taifa kubwa yenye nguvu na watu wengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe ujibu, ukaseme mbele za BWANA, Mungu wako, Baba yangu alikuwa Mwarami karibu na kupotea, akashuka Misri, akakaa huko ugenini, nao ni wachache hesabu yao; akawa taifa kubwa huko, yenye nguvu na watu wengi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
utasema maneno haya mbele ya Yawe, Mungu wako: ‘Baba yangu alikuwa Musuria aliyetangatanga huko na huko, kisha akashuka kwenda Misri akaishi huko kama mugeni. Yeye na jamaa yake walikuwa watu wachache tu walipokuwa huko, lakini wakakuwa taifa kubwa lenye nguvu na watu wengi.