Deuteronomy 27:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Juu yake mtaandika maneno yote ya sheria zote hizi, mtakapoingia katika nchi inayotiririka maziwa na asali ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa wazee wenu, aliwaahidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Andikeni juu yake maneno yote ya sheria hii wakati mtakapokuwa mmevuka na kuingia katika nchi anayowapa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, nchi inayotiririka maziwa na asali, kama vile Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
uyaandike maneno yote ya torati hii juu yake, utakapokwisha kuvuka; ili upate kuingia nchi akupayo Bwana, Mungu wako, nchi imiminikayo maziwa na asali, kama alivyokuahidi Bwana, Mungu wa baba zako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Juu yake mtaandika maneno yote ya sheria zote hizi, mtakapoingia katika nchi inayotiririka maziwa na asali ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa wazee wenu, aliwaahidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Andikeni juu yake maneno yote ya sheria hii wakati mtakapokuwa mmevuka na kuingia katika nchi awapayo BWANA Mungu wenu, nchi itiririkayo maziwa na asali, kama vile BWANA, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Andikeni juu yake maneno yote ya sheria hii wakati mtakapokuwa mmevuka na kuingia katika nchi awapayo bwana Mwenyezi Mungu wenu, nchi itiririkayo maziwa na asali, kama vile bwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
uyaandike maneno yote ya torati hii juu yake, utakapokwisha kuvuka; ili upate kuingia nchi akupayo BWANA, Mungu wako, nchi imiminikayo maziwa na asali, kama alivyokuahidi BWANA, Mungu wa baba zako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Juu yake mtaandika maneno yote ya sheria zote hizi, mtakapoingia katika nchi inayotiririka maziwa na asali ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa wazee wenu, aliwaahidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha uyaandike maneno yote ya Maonyo haya utakapokwisha kuvuka, kusudi upate kuingia katika nchi hiyo, Bwana Mungu wako atakayokupa. Nayo ni nchi ichuruzikayo maziwa na asali, kama Bwana Mungu wa baba zako alivyokuambia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
uyaandike maneno yote ya torati hii juu yake, utakapokwisha kuvuka; ili upate kuingia nchi akupayo BWANA, Mungu wako, nchi imiminikayo maziwa na asali, kama alivyokuahidi BWANA, Mungu wa baba zako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Juu yake mutaandika maneno yote ya sheria hizi zote, mutakapoingia katika inchi ile inayotiririka maziwa na asali, ambayo Yawe, Mungu wa wazee wenu, aliwaahidi.