Deuteronomy 28:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu atawafanikisha kwa wingi: Watoto, mifugo na mavuno shambani katika nchi aliyowaapia wazee wenu kuwa atawapeni,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu atakupa kustawi kwa wingi, katika tunda la uzao wa tumbo lako, katika wanyama wachanga wa mifugo yako na katika mazao ya ardhi yako, katika nchi aliyowaapia baba zako kukupa wewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako kwamba atakupa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu atawafanikisha kwa wingi: watoto, mifugo na mavuno shambani katika nchi aliyowaapia wazee wenu kuwa atawapeni,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA atakupa kustawi kwa wingi, katika tunda la uzao wa tumbo lako, katika wanyama wachanga wa mifugo yako na katika mazao ya ardhi yako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana atakupa kustawi kwa wingi, katika tunda la uzao wa tumbo lako, katika wanyama wachanga wa mifugo yako na katika mazao ya ardhi yako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwapa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako kwamba atakupa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu atawafanikisha kwa wingi: Watoto, mifugo na mavuno shambani katika nchi aliyowaapia wazee wenu kuwa atawapeni,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Bwana atakufurikishia mema: mazao ya tumbo lako na mazao ya nyama wako wa kufuga na mazao ya mashamba yako katika hiyo nchi, Bwana aliyowaapia baba zako kukupa wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako kwamba atakupa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe atawafanikisha kwa wingi: watoto, mifugo na mavuno katika shamba katika inchi aliyowaapia wazee wenu kwamba atawapa.