Deuteronomy 28:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini kama hamtaitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, au msipokuwa waangalifu kutekeleza amri zake zote na masharti ninayowaamuru leo, basi mtapatwa na laana hizi zote:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kama hutamtii Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na kuzishika kwa makini amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini kama hamtaitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, au msipokuwa waangalifu kutekeleza amri zake zote na masharti ninayowaamuru leo, basi mtapatwa na laana hizi zote:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, kama hutamtii BWANA Mungu wako na kuzishika kwa bidii amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, kama hutamtii bwana Mwenyezi Mungu wako na kuzishika kwa bidii amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini itakuwa usipotaka kuisikiliza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini kama hamtaitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, au msipokuwa waangalifu kutekeleza amri zake zote na masharti ninayowaamuru leo, basi mtapatwa na laana hizi zote:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini usipoisikia sauti ya Bwana Mungu wako, usiyaangalie na kuyafanya maagizo yake yote na maongozi yake yote, mimi ninayokuagiza leo, ndipo, yatakapokujia haya maapizo yote na kukupata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Lakini kama hamutaitii sauti ya Yawe, Mungu wenu, kama hamutakuwa waangalifu kushika amri zake zote na masharti ninayowaamuru leo, basi mutapatwa na laana hizi zote: