Deuteronomy 28:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu atawashambulia kwa kifua kikuu, homa, majipu, joto kali, ukame, dhoruba na ukungu; mambo hayo yatawaandama mpaka mmeangamia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu atakupiga kwa magonjwa ya kudhoofisha, kwa homa na kuwashwa, hari na kwa ukame, kutu na kuwa na uchungu ambavyo vitakupiga hadi uangamie.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu atawashambulia kwa kifua kikuu, homa, majipu, joto kali, ukame, dhoruba na ukungu; mambo hayo yatawaandama mpaka mmeangamia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA atakupiga kwa magonjwa ya kudhoofisha, kwa homa na kuwashwa, hari na kwa ukame, kutu na kuwa na uchungu ambavyo vitakupiga mpaka uangamie.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana atakupiga kwa magonjwa ya kudhoofisha, kwa homa na kuwashwa, hari na kwa ukame, kutu na kuwa na uchungu ambavyo vitakupiga mpaka uangamie.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa joto jingi, na kwa upanga, na kwa ukame, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu atawashambulia kwa kifua kikuu, homa, majipu, joto kali, ukame, dhoruba na ukungu; mambo hayo yatawaandama mpaka mmeangamia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana atakupiga kwa kifua kikuu na kwa homa na kwa kidingapopo na kwa kipindu na kwa upanga na kwa jua kali na kwa kunyausha ngano; haya yatakuhangaisha wewe, hata uangamie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe atawashambulia kwa kifua kikuu, homa, majipu, joto kali, ukavu, zoruba na ukungu; mambo hayo yatawaandama mpaka muangamie.