Deuteronomy 28:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maiti zenu zitakuwa chakula cha ndege wala hapatakuwa na mtu atakayewafukuza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mizoga yenu itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi, wala hapatakuwa na mtu yeyote wa kuwafukuza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maiti zenu zitakuwa chakula cha ndege wala hapatakuwa na mtu atakayewafukuza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mizoga yenu itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi, wala hapatakuwepo mtu ye yote wa kuwafukuza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mizoga yenu itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi, wala hapatakuwepo mtu yeyote wa kuwafukuza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maiti zenu zitakuwa chakula cha ndege wala hapatakuwa na mtu atakayewafukuza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mzoga wako utaliwa na ndege wote wa angani na nyama wa huku nchini, nao hawataona atakayewaamia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maiti zenu zitakuwa chakula cha ndege wala hakutakuwa mutu atakayewafukuza.