Deuteronomy 28:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtakwenda kwa kupapasapapasa mchana kama vipofu wala hamtafanikiwa katika shughuli zenu. Mtakuwa mkidhulumiwa kila mara na hakutakuwa na mtu wa kuwasaidieni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Adhuhuri utapapasapapasa kama kipofu gizani. Hutafanikiwa katika lolote ufanyalo; siku baada ya siku utadhulumiwa na kunyang’anywa, wala hakuna yeyote atakayekuokoa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtakwenda kwa kupapasapapasa mchana kama vipofu wala hamtafanikiwa katika shughuli zenu. Mtakuwa mkidhulumiwa kila mara na hakutakuwa na mtu wa kuwasaidieni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wa adhuhuri utapapasapapasa huko na huko kama mtu kipofu katika giza. Hutafanikiwa katika lo lote ufanyalo; siku baada ya siku utaonewa na kunyang'anywa, wala hakuna ye yote atakayekuokoa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wa adhuhuri utapapasapapasa huku na huko kama mtu kipofu katika giza. Hutafanikiwa katika lolote ufanyalo; siku baada ya siku utaonewa na kunyang’anywa, wala hakuna yeyote atakayekuokoa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
utakwenda kwa kupapasapapasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe siku zote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtakwenda kwa kupapasapapasa mchana kama vipofu wala hamtafanikiwa katika shughuli zenu. Mtakuwa mkidhulumiwa kila mara na hakutakuwa na mtu wa kuwasaidieni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe utakuwa ukipapasapapasa na mchana, kama kipofu anavyopapasa gizani, lakini hutafanikiwa katika njia zako, utakaa siku zote ukikorofishwa na kunyang'anywa pasipo kuona mwokozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutakwenda kwa kupapasapapasa muchana kama vipofu wala hamutafanikiwa katika shuguli zenu. Mutakuwa munateswa kila mara na hakutakuwa mutu wa kuwasaidia.