Deuteronomy 28:45 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Hayo yote yatawapateni nyinyi na kuwaandama mpaka muangamizwe kwa kuwa hamkutii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu kuhusu kushika amri zake na masharti aliyowapa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Laana hizi zote zitakuja juu yako. Zitakufuatia na kukupata hadi uangamizwe, kwa sababu hukumtii Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake aliyokupa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Hayo yote yatawapateni nyinyi na kuwaandama mpaka muangamizwe kwa kuwa hamkutii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu kuhusu kushika amri zake na masharti aliyowapa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Laana hizi zote zitakuja juu yako. Zitakufuatia na kukupata mpaka uangamizwe, kwa sababu hukumtii BWANA Mungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake aliyokupa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Laana hizi zote zitakuja juu yako. Zitakufuatia na kukupata mpaka uangamizwe, kwa sababu hukumtii bwana Mwenyezi Mungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake aliyokupa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiliza sauti ya BWANA, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Hayo yote yatawapateni nyinyi na kuwaandama mpaka muangamizwe kwa kuwa hamkutii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu kuhusu kushika amri zake na masharti aliyowapa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya maapizo yote yatakujia, yakuhangaishe; lakini yatakupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikia sauti ya Bwana Mungu wako na kuyaangalia maagizo yake na maongozi yake, aliyokuagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Hayo yote yatawapata ninyi na kuwaandama mpaka muangamie kwa sababu hamukutii sauti ya Yawe, Mungu wenu, juu ya kushika amri zake na masharti aliyowapa.