Deuteronomy 28:53 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati wa kuzingirwa na kutaabishwa na maadui wenu, mtakula watoto wenu ambao Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu amewapeni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utakula uzao wa tumbo lako, nyama ya wana wako wa kiume na wa kike, ambao Mwenyezi Mungu, Mungu wako, amekupa, kwa sababu ya mateso yale adui zako watakayokuletea wakati wa kukuzingira.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utakula uzao wa tumbo lako mwenyewe, nyama ya wana wako na binti zako aliokupa Bwana, Mungu wako; katika mazingirwa na katika mkazo utakaokazwa na adui zako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati wa kuzingirwa na kutaabishwa na maadui wenu, mtakula watoto wenu ambao Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu amewapeni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utakula uzao wa tumbo lako, nyama ya wana wako na binti zako ambao BWANA Mungu wako amekupa, kwa sababu ya mateso yale adui zako watakayokuletea wakati wa kukuzingira.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utakula uzao wa tumbo lako, nyama ya wana wako na binti zako ambao bwana Mwenyezi Mungu wako amekupa, kwa sababu ya mateso yale adui zako watakayokuletea wakati wa kukuzingira.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe utakula uzao wa tumbo lako mwenyewe, nyama ya wana wako na binti zako aliokupa BWANA, Mungu wako; katika kuzingirwa na katika mkazo utakaokazwa na adui zako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati wa kuzingirwa na kutaabishwa na maadui wenu, mtakula watoto wenu ambao Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu amewapeni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe kwa kusongeka na kwa kuhangaika utayala mazao ya tumbo lako, maana nyama zao wanao wa kiume na wa kike, Bwana Mungu wako atakaokupa; itakuwa hapo, adui zako watakapokuhangaisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utakula uzao wa tumbo lako mwenyewe, nyama ya wana wako na binti zako aliokupa BWANA, Mungu wako; katika mazingirwa na katika mkazo utakaokazwa na adui zako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati wa kuzungukwa na kutaabishwa na waadui zenu, mutakula watoto wenu ambao Yawe, Mungu wenu, amewapa.