Deuteronomy 28:63 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama vile Mwenyezi-Mungu alivyopendezwa kuwafanikisha na kuwafanya kuwa wengi, vivyo hivyo Mwenyezi-Mungu atapendezwa kuwaletea maafa na kuwaangamiza. Nanyi mtaondolewa katika nchi hiyo ambayo mnakwenda kuimiliki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama ilivyompendeza Mwenyezi Mungu kuwafanya ninyi mstawi na kuongezeka kwa idadi, ndivyo itakavyompendeza kuwaharibu na kuwaangamiza ninyi. Mtang’olewa kutoka nchi mnayoiingia kuimiliki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi Bwana juu yenu kwa kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi Bwana juu yenu kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi mwingiayo kuimiliki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama vile Mwenyezi-Mungu alivyopendezwa kuwafanikisha na kuwafanya kuwa wengi, vivyo hivyo Mwenyezi-Mungu atapendezwa kuwaletea maafa na kuwaangamiza. Nanyi mtaondolewa katika nchi hiyo ambayo mnakwenda kuimiliki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama ilivyompendeza BWANA kuwafanya ninyi mstawi na kuongezeka kwa idadi, ndivyo itakavyompendeza kuwaharibu na kuwaangamiza ninyi. Mtang'olewa kutoka katika nchi mnayoiingia kuimiliki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama ilivyompendeza bwana kuwafanya ninyi mstawi na kuongezeka kwa idadi, ndivyo itakavyompendeza kuwaharibu na kuwaangamiza ninyi. Mtang’olewa kutoka nchi mnayoiingia kuimiliki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi BWANA juu yenu kwa kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi BWANA juu yenu kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi mwingiayo kuimiliki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama vile Mwenyezi-Mungu alivyopendezwa kuwafanikisha na kuwafanya kuwa wengi, vivyo hivyo Mwenyezi-Mungu atapendezwa kuwaletea maafa na kuwaangamiza. Nanyi mtaondolewa katika nchi hiyo ambayo mnakwenda kuimiliki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama Bwana alivyofurahia kuwafanyizia mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo, Bwana atakavyofurahia kuwapoteza ninyi na kuwaangamiza, mng'olewe katika hiyo nchi, wewe unakokwenda sasa kuichukua, iwe yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi BWANA juu yenu kwa kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi BWANA juu yenu kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi mwingiayo kuimiliki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama vile Yawe alivyopendezwa kuwafanikisha na kuwafanya kuwa wengi, ni vile vile Yawe atapendezwa kuwaletea hasara na kuwaangamiza. Nanyi mutaondolewa katika inchi hiyo ambayo munakwenda kuirizi.