Deuteronomy 28:67 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mioyo yenu itajaa woga wa kila mtakachoona. Asubuhi mtasema, ‘Laiti ingekuwa jioni,’ jioni itakapofika mtasema, ‘Laiti ingekuwa asubuhi.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Asubuhi utasema hivi, “Laiti ingekuwa jioni!” Jioni utasema, “Laiti ingekuwa asubuhi,” kwa sababu ya hofu ile itakayojaza moyo wako na vitu vile macho yako yatakavyoviona.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mioyo yenu itajaa woga wa kila mtakachoona. Asubuhi mtasema, ‘Laiti ingekuwa jioni,’ jioni itakapofika mtasema, ‘Laiti ingekuwa asubuhi.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wa asubuhi utasema hivi, “Laiti ingekuwa jioni!” Jioni utasema, “Laiti ingekuwa asubuhi,” kwa sababu ya hofu ile itakayojaza moyo wako na vitu vile macho yako yatakavyoviona.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wa asubuhi utasema hivi, “Laiti ingekuwa jioni!” Jioni utasema, “Laiti ingekuwa asubuhi,” kwa sababu ya hofu ile itakayojaza moyo wako na vitu vile macho yako yatakavyoviona.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakayoona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mioyo yenu itajaa woga wa kila mtakachoona. Asubuhi mtasema, ‘Laiti ingekuwa jioni,’ jioni itakapofika mtasema, ‘Laiti ingekuwa asubuhi.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asubuhi utasema: Laiti iwe jioni! napo jioni utasema: Laiti iwe asubuhi! Kwani moyo wako utakaa kiwogawoga kwa ajili ya hayo, utakayoyaogopa, na kuyaona yale mambo, macho yako yatakayoyaona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mioyo yenu itajaa woga wa kila kitu mutakachoona. Asubui mutasema ‘Heri ingekuwa magaribi’; magaribi itakapofika mutasema ‘Heri ingekuwa asubui’.