Deuteronomy 29:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Haya ni maneno ya agano ambalo Mwenyezi-Mungu aliwaamuru Mose kufanya na Waisraeli katika nchi ya Moabu, licha ya agano Mwenyezi-Mungu alilofanya nao mlimani Horebu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya ndio maneno ya agano Mwenyezi Mungu alilomwagiza Musa kufanya na Waisraeli huko Moabu, yakiwa nyongeza ya agano alilofanya nao huko Horebu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya ndiyo maneno ya agano Bwana alilomwamuru Musa alifanye na wana wa Israeli katika nchi ya Moabu, pamoja na agano alilofanya nao Horebu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Haya ni maneno ya agano ambalo Mwenyezi-Mungu aliwaamuru Mose kufanya na Waisraeli katika nchi ya Moabu, licha ya agano Mwenyezi-Mungu alilofanya nao mlimani Horebu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya ndiyo maneno ya Agano BWANA aliyomwagiza Mose kufanya na Waisraeli huko Moabu, kuwa nyongeza ya Agano alilofanya nao huko Horebu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya ndiyo maneno ya Agano bwana aliyomwagiza Musa kufanya na Waisraeli huko Moabu, kuwa nyongeza ya Agano alilofanya nao huko Horebu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya ndiyo maneno ya agano BWANA alilomwamuru Musa alifanye na wana wa Israeli katika nchi ya Moabu, pamoja na agano alilofanya nao Horebu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Haya ni maneno ya agano ambalo Mwenyezi-Mungu aliwaamuru Mose kufanya na Waisraeli katika nchi ya Moabu, licha ya agano Mwenyezi-Mungu alilofanya nao mlimani Horebu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya ndiyo maneno ya Agano, Bwana aliyomwagiza Mose kulifanya na wana wa Isiraeli katika nchi ya Moabu, tena liko Agano lile, alilolifanya nao mlimani kwa Horebu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya ndiyo maneno ya agano BWANA alilomwamuru Musa alifanye na wana wa Israeli katika nchi ya Moabu, pamoja na agano alilofanya nao Horebu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akawaita pamoja Waisraeli wote akawaambia: “Muliona ninyi wenyewe jinsi Yawe alivyomutendea mufalme wa Misri, wakubwa, watumishi wake na inchi yake yote.