Deuteronomy 29:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama baada ya kusikia maneno ya agano hili ambayo mmeapishwa, halafu mtu akajiamini mwenyewe moyoni mwake na kusema atakuwa salama, hata kama atafuata ukaidi wake mwenyewe, hiyo itawaangamiza wote, wabaya na wema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu wa namna hii asikiapo maneno ya kiapo hiki, hujibariki mwenyewe, na kisha hufikiri, “Nitakuwa salama, hata nikiendelea kuifuata njia yangu mwenyewe.” Hili litaleta maafa juu ya nchi iliyoneshewa sawasawa na nchi kame.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ikawa asikiapo maneno ya laana hii, ajibarikie mtu huyo moyoni mwake, na kusema, Nitakuwa katika amani, nijapotembea katika upotoe wa moyo wangu kwa kuangamiza mbichi na kavu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama baada ya kusikia maneno ya agano hili ambayo mmeapishwa, halafu mtu akajiamini mwenyewe moyoni mwake na kusema atakuwa salama, hata kama atafuata ukaidi wake mwenyewe, hiyo itawaangamiza wote, wabaya na wema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati mtu wa namna hii asikiapo maneno ya kiapo hiki, hujibariki mwenyewe na kisha hufikiri, “Nitakuwa salama, hata kama nikiendelea kuifuata njia yangu mwenyewe.” Hili litaleta maafa juu ya nchi iliyonyeshewa sawasawa na nchi kame.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati mtu wa namna hii asikiapo maneno ya kiapo hiki, hujibariki mwenyewe na kisha hufikiri, “Nitakuwa salama, hata kama nikiendelea kuifuata njia yangu mwenyewe.” Hili litaleta maafa juu ya nchi iliyonyeshewa sawasawa na nchi kame.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ikawa asikiapo maneno ya laana hii, ajibarikie mtu huyo moyoni mwake, na kusema, Nitakuwa katika amani, nijapotembea katika upotovu wa moyo wangu kwa kuangamiza mbichi na kavu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama baada ya kusikia maneno ya agano hili ambayo mmeapishwa, halafu mtu akajiamini mwenyewe moyoni mwake na kusema atakuwa salama, hata kama atafuata ukaidi wake mwenyewe, hiyo itawaangamiza wote, wabaya na wema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu aliye hivyo atakapoyasikia maneno ya kiapizo hiki asijibariki mwenyewe moyoni mwake kwamba: Nitapata kutengemana, ijapo niendelee kuufuata ushupavu wa moyo wangu, kusudi niyapokonye mabichi na makavu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ikawa asikiapo maneno ya laana hii, ajibarikie mtu huyo moyoni mwake, na kusema, Nitakuwa katika amani, nijapotembea katika upotoe wa moyo wangu kwa kuangamiza mbichi na kavu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe hatasamehe mutu huyo, nayo hasira ya Yawe na wivu wake vitamuwakia mutu huyo. Laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki zitamupata, naye Yawe atafuta kabisa jina la mutu huyo kutoka katika dunia.