Deuteronomy 29:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose aliwaita pamoja Waisraeli wote akawaambia, “Mliona nyinyi wenyewe jinsi Mwenyezi-Mungu alivyomtendea mfalme wa Misri, maofisa, watumishi wake na nchi yake yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa akawaita Waisraeli wote, akawaambia: Macho yenu yameona yale yote Mwenyezi Mungu aliyofanya kwa Mfalme Farao huko Misri, kwa maafisa wake wote na kwa nchi yake yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akawaita Israeli wote akawaambia, Mmeyaona yote Bwana aliyomfanya Farao katika nchi ya Misri mbele ya macho yenu, yeye na watumwa wake wote, na nchi yake yote;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose aliwaita pamoja Waisraeli wote akawaambia, “Mliona nyinyi wenyewe jinsi Mwenyezi-Mungu alivyomtendea mfalme wa Misri, maofisa, watumishi wake na nchi yake yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose akawaita Waisraeli wote akawaambia: Macho yenu yameona yale yote BWANA aliyofanya kwa Mfalme Farao huko Misri, kwa maafisa wake wote na kwa nchi yake yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa akawaita Waisraeli wote akawaambia: Macho yenu yameona yale yote bwana aliyofanya kwa Mfalme Farao huko Misri, kwa maafisa wake wote na kwa nchi yake yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akawaita Israeli wote akawaambia, Mmeyaona yote BWANA aliyomfanya Farao katika nchi ya Misri mbele ya macho yenu, yeye na watumwa wake wote, na nchi yake yote;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose aliwaita pamoja Waisraeli wote akawaambia, “Mliona nyinyi wenyewe jinsi Mwenyezi-Mungu alivyomtendea mfalme wa Misri, maofisa, watumishi wake na nchi yake yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose akawaita Waisiraeli wote, akawaambia: Ninyi mliona yote, Bwana aliyomfanyizia Farao, nao watumishi wake wote na wenyeji wote wa nchi yake machoni penu katika nchi ya Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akawaita Israeli wote akawaambia, Mmeyaona yote BWANA aliyomfanya Farao katika nchi ya Misri mbele ya macho yenu, yeye na watumwa wake wote, na nchi yake yote;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muliona majaribu makubwa, vitambulisho na maajabu aliyotenda.