Deuteronomy 29:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu hatasamehe mtu huyo, nayo hasira ya Mwenyezi-Mungu na wivu wake vitamwakia mtu huyo; laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki zitamjia, naye Mwenyezi-Mungu atalifuta kabisa jina la mtu huyo kutoka duniani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu kamwe hatakuwa radhi kumsamehe, ghadhabu na wivu wa Mungu vitawaka dhidi ya mtu huyo. Laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki zitamwangukia na Mwenyezi Mungu atafuta jina lake chini ya mbingu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya Bwana na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na Bwana atalifuta jina lake chini ya mbingu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu hatasamehe mtu huyo, nayo hasira ya Mwenyezi-Mungu na wivu wake vitamwakia mtu huyo; laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki zitamjia, naye Mwenyezi-Mungu atalifuta kabisa jina la mtu huyo kutoka duniani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA kamwe hatakuwa radhi kumsamehe, ghadhabu na wivu wa Mungu vitawaka dhidi ya mtu huyo. Laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki zitamwangukia na BWANA atafuta jina lake chini ya mbingu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana kamwe hatakuwa radhi kumsamehe, ghadhabu na wivu wa Mungu vitawaka dhidi ya mtu huyo. Laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki zitamwangukia na bwana atafuta jina lake chini ya mbingu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya BWANA na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na BWANA atalifuta jina lake chini ya mbingu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu hatasamehe mtu huyo, nayo hasira ya Mwenyezi-Mungu na wivu wake vitamwakia mtu huyo; laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki zitamjia, naye Mwenyezi-Mungu atalifuta kabisa jina la mtu huyo kutoka duniani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aliye hivyo Bwana atakataa kabisa kumwondolea mabaya, ila hapo ndipo, makali ya Bwana pamoja na wivu wake yatakapowaka moto wenye moshi kwa kumkasirikia huyo mtu, navyo viapizo vyote vilivyoandikwa humu kitabuni vitamkalia, naye Bwana atalifuta jina lake chini ya mbingu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya BWANA na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na BWANA atalifuta jina lake chini ya mbingu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe atamutenga kutoka kati ya makabila yote ya Israeli apatwe na hasara kufuatana na laana zote za agano zilizoandikwa katika kitabu hiki.