Deuteronomy 29:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu atamtenga kutoka miongoni mwa makabila yote ya Israeli apatwe na maafa kufuatana na laana zote za agano zilizoandikwa katika kitabu hiki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu atamtwaa peke yake kutoka makabila ya Israeli kwa maangamizi, kulingana na laana zote za agano zilizoandikwa kwenye Kitabu hiki cha Torati.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana atamtenga kwa uovu, kutoka kabila zote za Israeli, kwa laana zote za agano lililoandikwa katika chuo hiki cha torati.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu atamtenga kutoka miongoni mwa makabila yote ya Israeli apatwe na maafa kufuatana na laana zote za agano zilizoandikwa katika kitabu hiki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA atamtwaa peke yake kutoka makabila ya Israeli kwa maangamizo, kulingana na laana zote za Agano zilizoandikwa kwenye Kitabu hiki cha Sheria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana atamtwaa peke yake kutoka makabila ya Israeli kwa maangamizo, kulingana na laana zote za Agano zilizoandikwa kwenye Kitabu hiki cha Torati.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA atamtenga kwa uovu, kutoka kabila zote za Israeli, kwa laana zote za agano lililoandikwa katika kitabu hiki cha torati.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu atamtenga kutoka miongoni mwa makabila yote ya Israeli apatwe na maafa kufuatana na laana zote za agano zilizoandikwa katika kitabu hiki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena Bwana atamtenga na kumtoa katika mashina yote ya Isiraeli, apatwe na mabaya, vimtimilikie viapizo vyote vya Agano hili lililoandikwa katika kitabu cha Maonyo haya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA atamtenga kwa uovu, kutoka kabila zote za Israeli, kwa laana zote za agano lililoandikwa katika chuo hiki cha torati.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika vizazi vinavyokuja, wazao wenu na wageni kutoka inchi ya mbali wataona jinsi Yawe alivyoletea inchi hii hasara na mateso.