Deuteronomy 29:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Imejaa madini ya kiberiti na chumvi, imeteketea na kuwa tupu, haikupandwa mbegu na haioti chochote. Ni kama ilivyokuwa wakati Mwenyezi-Mungu alipoangamiza Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, kwa hasira yake kali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nchi yote itakuwa jaa linaloungua la chumvi na kiberiti: hakutakuwa kilichopandwa, hakutakuwa kinachochipua, wala hakutakuwa na mimea inayoota juu yake. Itakuwa kama maangamizi ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, ambazo Mwenyezi Mungu aliangamiza kwa hasira kali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, aliyoipindua Bwana kwa ghadhabu yake na hasira zake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
imejaa madini ya kiberiti na chumvi, imeteketea na kuwa tupu, haikupandwa mbegu na haioti chochote. Ni kama ilivyokuwa wakati Mwenyezi-Mungu alipoangamiza Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, kwa hasira yake kali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nchi yote itakuwa jaa linaloungua la chumvi na kiberiti: hakutakuwa kilichopandwa, hakutakuwa kinachochipua, wala hakutakuwa mimea inayoota juu yake. Itakuwa kama maangamizo ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, ambazo BWANA aliangamiza kwa hasira kali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nchi yote itakuwa jaa linaloungua la chumvi na kiberiti: hakutakuwa kilichopandwa, hakutakuwa kinachochipua, wala hakutakuwa mimea inayoota juu yake. Itakuwa kama maangamizo ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, ambazo bwana aliangamiza kwa hasira kali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, aliyoipindua BWANA kwa ghadhabu yake na hasira zake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Imejaa madini ya kiberiti na chumvi, imeteketea na kuwa tupu, haikupandwa mbegu na haioti chochote. Ni kama ilivyokuwa wakati Mwenyezi-Mungu alipoangamiza Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, kwa hasira yake kali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwani nchi yake nzima ataiteketeza kwa mawe ya kiberiti na kwa chumvi, isiweze kupandwa wala kuotesha kijiti, wala majani yo yote yasiweze kumea huko, mwangamizo wake uwe kama ule wa Sodomu na wa Gomora, nao wa Adima na wa Seboimu, Bwana aliyoiangamiza kwa makali yake yaliyowaka moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, aliyoipindua BWANA kwa ghadhabu yake na hasira zake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata mataifa yote yatasema: ‘Kwa nini Yawe ameitendea hivyo inchi hii? Hasira hii kubwa ina maana gani?’