Deuteronomy 3:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yairi, mtu wa kabila la Manase, alichukua eneo lote la nchi ya Argobu, yaani Bashani, hadi kwenye mpaka wa Geshuri na Maaka. Vijiji vyote alivipa jina lake, na hadi leo vinajulikana kama vijiji Hawoth-yairi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yairi, mzao wa kabila la Manase, alichukua eneo lote la nchi ya Argobu hadi kufikia mpaka wa Wageshuri na Wamaaka, ukaitwa kwa jina lake; kwa hiyo hadi leo Bashani inaitwa Hawoth-Yairi.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yairi, mwana wa Manase, alitwaa nchi yote ya Argobu, hata mpaka wa Wageshuri na Wamaaka; akaziita nchi hizo Hawoth-yairi, kwa jina lake mwenyewe, hata hivi leo, maana, hizo nchi za Bashani.)
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yairi, mtu wa kabila la Manase, alichukua eneo lote la nchi ya Argobu, yaani Bashani, hadi kwenye mpaka wa Geshuri na Maaka. Vijiji vyote alivipa jina lake, na hadi leo vinajulikana kama vijiji Hawoth-yairi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yairi, mzao wa kabila la Manase, alichukuwa eneo lote la nchi ya Argobu hadi kufikia mpaka wa Wageshuri na Wamaaka, ukaitwa kwa jina lake; kwa hiyo mpaka leo hii Bashani inaitwa Hawath-Yairi.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yairi, mzao wa kabila la Manase, alichukua eneo lote la nchi ya Argobu hadi kufikia mpaka wa Wageshuri na Wamaaka, ukaitwa kwa jina lake; kwa hiyo mpaka leo hii Bashani inaitwa Hawoth-Yairi.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yairi, mwana wa Manase, alitwaa nchi yote ya Argobu, hata mpaka wa Wageshuri na Wamaaka; akaziita nchi hizo Hawoth-yairi, kwa jina lake mwenyewe, hata hivi leo, yaani, hizo nchi za Bashani.)
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yairi, mtu wa kabila la Manase, alichukua eneo lote la nchi ya Argobu, yaani Bashani, hadi kwenye mpaka wa Geshuri na Maaka. Vijiji vyote alivipa jina lake, na hadi leo vinajulikana kama vijiji Hawoth-yairi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yairi, mwana wa Manase, alikichukua kile kipande chote cha Argobu hata mpakani kwa Wagesuri na Wamakati, akaziita hizo nchi za Basani kwa jina lake Mahema ya Yairi; ndivyo, zinavyoitwa hata leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yairi, mwana wa Manase, alitwaa nchi yote ya Argobu, hata mpaka wa Wageshuri na Wamaaka; akaziita nchi hizo Hawoth-yairi, kwa jina lake mwenyewe, hata hivi leo, maana, hizo nchi za Bashani.)
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yairi, mutu wa kabila la Manase, alitwaa eneo lote la inchi ya Argobu, ni kusema Basani, mpaka kwenye mupaka wa Gesuri na Maka. Vijiji vyote alivipa jina lake, na mpaka leo vinajulikana kama vile ‘Vijiji vya Yairi’.