Deuteronomy 3:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wasaidieni ndugu zenu Waisraeli mpaka Mwenyezi-Mungu atakapowajalia watulie mahali pao kama nanyi mlivyotulia, yaani nao pia waimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapatia huko ngambo ya Yordani. Baada ya hayo, mtaweza kurejea katika nchi yenu hii ambayo nimewapeni iwe yenu!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
hadi hapo Mwenyezi Mungu atakapowapa ndugu zenu kupumzika kama alivyowapa ninyi, wao pia wamiliki ile nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawapa, ng’ambo ya Yordani. Baada ya hapo, kila mmoja wenu anaweza kurudi kwenye milki niliyowapa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hata Bwana awapumzishe ndugu zenu kama ninyi, nao pia waimiliki nchi wapewayo na Bwana, Mungu wenu, ng'ambo ya Yordani; ndipo mtakaporudi kila mmoja aende katika milki yake niliyowapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wasaidieni ndugu zenu Waisraeli mpaka Mwenyezi-Mungu atakapowajalia watulie mahali pao kama nanyi mlivyotulia, yaani nao pia waimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapatia huko ng'ambo ya Yordani. Baada ya hayo, mtaweza kurejea katika nchi yenu hii ambayo nimewapeni iwe yenu!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mpaka hapo BWANA atakapowapa ndugu zenu kupumzika kama alivyowapa ninyi, wao pia wamiliki ile nchi ambayo BWANA Mungu wenu anawapa, ng'ambo ya Yordani. Baada ya hapo, kila mmoja wenu anaweza kurudi kwenye milki niliyowapa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mpaka hapo bwana atakapowapa ndugu zenu kupumzika kama alivyowapa ninyi, wao pia wamiliki ile nchi ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa, ng’ambo ya Yordani. Baada ya hapo, kila mmoja wenu anaweza kurudi kwenye milki niliyowapa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hata BWANA awapumzishe ndugu zenu kama ninyi, nao pia waimiliki nchi wapewayo na BWANA, Mungu wenu, ng'ambo ya Yordani; ndipo mtakaporudi kila mmoja aende katika milki yake niliyowapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wasaidieni ndugu zenu Waisraeli mpaka Mwenyezi-Mungu atakapowajalia watulie mahali pao kama nanyi mlivyotulia, yaani nao pia waimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapatia huko ngambo ya Yordani. Baada ya hayo, mtaweza kurejea katika nchi yenu hii ambayo nimewapeni iwe yenu!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo, Bwana atakapowapatia ndugu zenu kutulia kama ninyi, nao watakapokwisha kuichukua nchi, Bwana Mungu wenu atakayowapa ng'ambo ya huko ya Yordani, ndipo, mtakaporudi kila mtu kwenye nchi yake, aliyoichukua, iwe yake, niliyowapa ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hata BWANA awapumzishe ndugu zenu kama ninyi, nao pia waimiliki nchi wapewayo na BWANA, Mungu wenu, ng’ambo ya Yordani; ndipo mtakaporudi kila mmoja aende katika milki yake niliyowapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muwasaidie wandugu zenu Waisraeli mpaka Yawe atakapowajalia watulie pahali pao kama vile nanyi mulivyotulia, ni kusema nao vilevile warizi inchi ambayo Yawe, Mungu wenu, anawapatia huko ngambo ya Yordani. Nyuma ya hayo, mutaweza kurudia katika inchi yenu hii ambayo nimewapa ikuwe yenu!’