Deuteronomy 3:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kisha nikamwamuru Yoshua, ‘Wewe umeona kwa macho yako mambo yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, amewatendea wafalme hawa wawili, Sihoni na Ogu; basi, yeye atawatendea vivyo hivyo wafalme wa nchi zote mtakazopitia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo nilimwamuru Yoshua, “Umejionea kwa macho yako mwenyewe yale yote ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewafanyia wafalme hawa wawili. Mwenyezi Mungu atazifanyia falme zote huko mnakoenda vivyo hivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikamwamuru Yoshua wakati huo, nikamwambia, Macho yako yameona yote aliyowatenda Bwana, Mungu wenu, wale wafalme wawili, navyo ndivyo atakavyoutenda Bwana kila ufalme huko uvukiako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kisha nikamwamuru Yoshua, ‘Wewe umeona kwa macho yako mambo yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, amewatendea wafalme hawa wawili, Sihoni na Ogu; basi, yeye atawatendea vivyo hivyo wafalme wa nchi zote mtakazopitia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo nilimwamuru Yoshua, “Umejionea kwa macho yako mwenyewe yale yote ambayo BWANA Mungu wenu amewafanyia wafalme hawa wawili. BWANA atazifanyia falme zote huko mnakokwenda vivyo hivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo nilimwamuru Yoshua, “Umejionea kwa macho yako mwenyewe yale yote ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu amewafanyia wafalme hawa wawili. bwana atazifanyia falme zote huko mnakokwenda vivyo hivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikamwamuru Yoshua wakati huo, nikamwambia, Macho yako yameona yote aliyowatenda BWANA, Mungu wenu, wale wafalme wawili, na ndivyo atakavyoutenda BWANA kila ufalme huko uvukiako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kisha nikamwamuru Yoshua, ‘Wewe umeona kwa macho yako mambo yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, amewatendea wafalme hawa wawili, Sihoni na Ogu; basi, yeye atawatendea vivyo hivyo wafalme wa nchi zote mtakazopitia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Yosua nikamwagiza siku hizo kwamba: Macho yako yameyaona yote, Bwama Mungu wetu aliyowafanyizia hao wafalme wawili; hivyo ndivyo, Bwana atakavyozifanyizia nchi zote za kifalme, utakazoziingia wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikamwamuru Yoshua wakati huo, nikamwambia, Macho yako yameona yote aliyowatenda BWANA, Mungu wenu, wale wafalme wawili, navyo ndivyo atakavyoutenda BWANA kila ufalme huko uvukiako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kisha nikamwamuru Yoshua: ‘Wewe umeona kwa macho yako mambo yote ambayo Yawe, Mungu wako, amewatendea wafalme hawa wawili, Sihoni na Ogi. Basi, yeye atawatendea vile vile wafalme wa inchi zote mutakazopitia.