Deuteronomy 3:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
‘Ee Bwana, Mwenyezi-Mungu, ninajua umenionesha mimi mtumishi wako mwanzo tu wa ukuu wako na uwezo wako. Maana, kuna mungu gani huko mbinguni au duniani awezaye kufanya mambo makuu na ya ajabu kama ulivyofanya wewe?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ee Bwana Mungu Mwenyezi, umemwonesha mtumishi wako ukuu wako na mkono wako wenye uweza. Kwa kuwa ni mungu yupi aliye mbinguni au duniani anayeweza kufanya kazi na matendo makuu kama ufanyayo wewe?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana Mungu, umeanza kumwonyesha mtumishi wako ukubwa wako, na mkono wako wa nguvu; kwani kuna mungu gani mbinguni au duniani awezaye kufanya mfano wa kazi zako, na mfano wa matendo yako yenye nguvu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
‘Ee Bwana, Mwenyezi-Mungu, ninajua umenionesha mimi mtumishi wako mwanzo tu wa ukuu wako na uwezo wako. Maana, kuna mungu gani huko mbinguni au duniani awezaye kufanya mambo makuu na ya ajabu kama ulivyofanya wewe?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ee BWANA Mwenyezi, umemwonyesha mtumishi wako ukuu wako na mkono wako wenye uweza. Kwa kuwa ni mungu yupi aliyeko mbinguni au duniani anayeweza kufanya kazi na matendo makuu kama ufanyayo wewe?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ee bwana Mwenyezi, umemwonyesha mtumishi wako ukuu wako na mkono wako wenye uweza. Kwa kuwa ni mungu yupi aliye mbinguni au duniani anayeweza kufanya kazi na matendo makuu kama ufanyayo wewe?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee BWANA Mungu, umeanza kumwonesha mtumishi wako ukuu wako, na mkono wako wa nguvu; kwani kuna mungu gani mbinguni au duniani awezaye kufanya mfano wa kazi zako, na mfano wa matendo yako yenye nguvu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
‘Ee Bwana, Mwenyezi-Mungu, ninajua umenionesha mimi mtumishi wako mwanzo tu wa ukuu wako na uwezo wako. Maana, kuna mungu gani huko mbinguni au duniani awezaye kufanya mambo makuu na ya ajabu kama ulivyofanya wewe?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mungu wangu, wewe umeanza kumwonyesha mtumishi wako ukuu wako na nguvu za mkono wako; kwani yuko Mungu gani mbinguni na duniani anayeweza kufanya matendo, kama hayo ya uwezo wako mwingi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee BWANA Mungu, umeanza kumwonyesha mtumishi wako ukubwa wako, na mkono wako wa nguvu; kwani kuna mungu gani mbinguni au duniani awezaye kufanya mfano wa kazi zako, na mfano wa matendo yako yenye nguvu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
‘Ee Bwana wetu Yawe, ninajua umenionyesha mimi mutumishi wako mwanzo tu wa ukubwa wako na uwezo wako. Maana, kuna mungu gani huko mbinguni au katika dunia anayeweza kufanya mambo makubwa na ya ajabu kama vile ulivyofanya wewe?