Deuteronomy 30:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akaendelea kusema, “Nimewapeni uchaguzi kati ya baraka na laana. Mambo hayo yote yakiwapata nanyi mkiyatafakari popote mlipo miongoni mwa mataifa ambamo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atakuwa amewatawanya,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baraka hizi zote pamoja na laana nilizoziweka mbele yako zitakapokujia, nawe ukazitafakari moyoni popote Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakapokutawanya miongoni mwa mataifa,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena itakuwa, mambo haya yote yatakapokujilia, baraka na laana nilizoweka mbele yako, nawe utakapozikumbuka kati ya mataifa yote, huko atakakokupeleka Bwana, Mungu wako,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akaendelea kusema, “Nimewapeni uchaguzi kati ya baraka na laana. Mambo hayo yote yakiwapata nanyi mkiyatafakari popote mlipo miongoni mwa mataifa ambamo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atakuwa amewatawanya,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati baraka hizi zote pamoja na laana nilizoziweka mbele yako zitakapokujia, nawe ukazitafakari moyoni popote BWANA Mungu wako atakapokutawanya miongoni mwa mataifa,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati baraka hizi zote pamoja na laana nilizoziweka mbele yako zitakapokujia, nawe ukazitafakari moyoni popote bwana Mwenyezi Mungu wako atakapokutawanya miongoni mwa mataifa,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena itakuwa, mambo haya yote yatakapokujilia, baraka na laana nilizoweka mbele yako, nawe utakapozikumbuka kati ya mataifa yote, huko atakakokupeleka BWANA, Mungu wako,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akaendelea kusema, “Nimewapeni uchaguzi kati ya baraka na laana. Mambo hayo yote yakiwapata nanyi mkiyatafakari popote mlipo miongoni mwa mataifa ambamo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atakuwa amewatawanya,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo yote yatakapokujia, hayo ya mbaraka nayo ya kiapizo, niliyoyaweka mbele yako, nawe utakapoyaingiza moyoni mwako katika wamizimu wote, Bwana Mungu wako atakapokukumba kwenda kwao,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena itakuwa, mambo haya yote yatakapokujilia, baraka na laana nilizoweka mbele yako, nawe utakapozikumbuka kati ya mataifa yote, huko atakakokupeleka BWANA, Mungu wako,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akaendelea kusema: “Baraka na laana hizi zote zitatimizwa. Mutafikiri juu ya mambo hayo wakati Yawe, Mungu wenu, atakuwa amewatawanya kati ya mataifa.