Deuteronomy 30:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama mkitii amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambazo ninawapa leo, mkampenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kufuata njia zake na kushika masharti na maagizo yake, basi, mtaishi na kuongezeka; naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawabariki katika nchi ambayo mnakwenda kuimiliki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninakuamuru leo kwamba umpende Mwenyezi Mungu, Mungu wako, utembee katika njia zake, na kutunza maagizo yake, amri na sheria zake; ndipo utakapoishi na kuongezeka, naye Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakubariki katika nchi unayoingia kuimiliki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda Bwana, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama mkitii amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambazo ninawapa leo, mkampenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kufuata njia zake na kushika masharti na maagizo yake, basi, mtaishi na kuongezeka; naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawabariki katika nchi ambayo mnakwenda kuimiliki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninakuamuru leo kwamba umpende BWANA Mungu wako, utembee katika njia zake, na kutunza maagizo yake, amri na sheria zake; ndipo utakapoishi na kuongezeka, naye BWANA Mungu wako atakubariki katika nchi unayoiingia kuimiliki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninakuamuru leo kwamba umpende bwana Mwenyezi Mungu wako, utembee katika njia zake, na kutunza maagizo yake, amri na sheria zake; ndipo utakapoishi na kuongezeka, naye bwana Mwenyezi Mungu wako atakubariki katika nchi unayoingia kuimiliki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda BWANA, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama mkitii amri za Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ambazo ninawapa leo, mkampenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kufuata njia zake na kushika masharti na maagizo yake, basi, mtaishi na kuongezeka; naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawabariki katika nchi ambayo mnakwenda kuimiliki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi ninakuagiza leo kumpenda Bwana Mungu wako na kuzishika njia zake na kuyaangalia maagizo yake na maongozi yake na maamuzi yake, ndipo, utakapopona, watu wako wawe wengi, naye Bwana Mungu wako atakubariki katika nchi hiyo, wewe unayokwenda kuichukia, iwe yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda BWANA, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mukitii amri za Yawe, Mungu wenu, ambazo ninawapa leo, mukimupenda Yawe, Mungu wenu, na kufuata njia zake na kushika amri, masharti na maagizo yake, basi, mutaishi na kuongezeka; naye Yawe, Mungu wenu, atawabariki katika inchi ambayo munakwenda kuirizi.