Deuteronomy 30:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mkimpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mkiitii sauti yake na kuambatana naye. Maana kufanya hivyo kunamaanisha kwamba mtapata maisha marefu na kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu aliwaahidi wazee wenu, Abrahamu, Isaka na Yakobo, kwamba atawapeni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na ili upate kumpenda Mwenyezi Mungu, Mungu wako, uisikilize sauti yake na kuambatana naye. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye uzima wako, na atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi aliyoapa kuwapa baba zako Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mkimpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mkiitii sauti yake na kuambatana naye. Maana kufanya hivyo kunamaanisha kwamba mtapata maisha marefu na kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu aliwaahidi wazee wenu, Abrahamu, Isaka na Yakobo, kwamba atawapeni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na ili upate kumpenda BWANA Mungu wako, uisikilize sauti yake na kuambatana naye. Kwa kuwa BWANA ndiye uzima wako, na atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi aliyoapa kuwapa baba zako Abrahamu, Isaki na Yakobo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na ili upate kumpenda bwana Mwenyezi Mungu wako, uisikilize sauti yake na kuambatana naye. Kwa kuwa bwana ndiye uzima wako, na atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi aliyoapa kuwapa baba zako Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani huo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mkimpenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mkiitii sauti yake na kuambatana naye. Maana kufanya hivyo kunamaanisha kwamba mtapata maisha marefu na kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu aliwaahidi wazee wenu, Abrahamu, Isaka na Yakobo, kwamba atawapeni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mkimpenda Bwana Mungu wenu, mwisikie sauti yake na kugandamana naye; kwani humu ndimo, yalimo maisha yako na wingi wa siku zako za kukaa katika hiyo nchi, Bwana aliyowaapia baba zako Aburahamu na Isaka na Yakobo kuwapa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumupende Yawe, Mungu wenu. Muitii sauti yake na kuambatana naye. Kama munafanya hivyo, mutapata maisha marefu na kuishi katika inchi ambayo Yawe aliwaahidi wazee wenu, Abrahamu, Isaka na Yakobo, kwamba atawapa.”