Deuteronomy 30:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
hapo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawarudishieni mema yenu na kuwahurumia na kuwakusanya tena kutoka katika mataifa ambamo atakuwa amewatawanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ndipo Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakapokurudisha kutoka utumwani na kukuhurumia, naye atakukusanya tena kutoka mataifa yote kule alikutawanya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo Bwana, Mungu wako, atakapougeuza utumwa wako, naye atakuhurumia, tena atarejea na kukukusanya kutoka mataifa yote, huko alikokutawanyia Bwana, Mungu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
hapo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawarudishieni mema yenu na kuwahurumia na kuwakusanya tena kutoka katika mataifa ambamo atakuwa amewatawanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ndipo BWANA Mungu wako atakapokurudisha kutoka utumwani na kukuhurumia, naye atakukusanya tena kutoka katika mataifa yote kule alikokutawanya wewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ndipo bwana Mwenyezi Mungu wako atakapokurudisha kutoka utumwani na kukuhurumia, naye atakukusanya tena kutoka mataifa yote kule alikutawanya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo BWANA, Mungu wako, atakapougeuza utumwa wako, naye atakuhurumia, tena atarejea na kukukusanya kutoka mataifa yote, huko alikokutawanyia BWANA, Mungu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
hapo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawarudishieni mema yenu na kuwahurumia na kuwakusanya tena kutoka katika mataifa ambamo atakuwa amewatawanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, Bwana Mungu wako atakapoyafungua mafungo yako kwa kukuhurumia, akukutanishe tena na kukutoa katika makabila yote, Bwana Mungu wako alikokutawanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo BWANA, Mungu wako, atakapougeuza utumwa wako, naye atakuhurumia, tena atarejea na kukukusanya kutoka mataifa yote, huko alikokutawanyia BWANA, Mungu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
hapo Yawe, Mungu wenu, atawarudishia mema yenu na kuwahurumia na kuwakusanya tena kutoka katika mataifa ambamo atakuwa amewatawanya.