Deuteronomy 31:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakusanye watu: Wanaume, wanawake, watoto na wageni wanaoishi katika miji yenu, ili kila mmoja asikie maneno haya ya kujifunza kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kuwa waangalifu kutekeleza maneno ya sheria hii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kusanya watu wote, wanaume, wanawake, watoto na wageni wanaoishi katika miji yenu, ili waweze kusikia na kujifunza kumcha Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kuzingatia maneno yote ya sheria hii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na kumcha Bwana, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakusanye watu: wanaume, wanawake, watoto na wageni wanaoishi katika miji yenu, ili kila mmoja asikie maneno haya ya kujifunza kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kuwa waangalifu kutekeleza maneno ya sheria hii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kusanya watu wote, wanaume, wanawake, watoto na wageni wanaoishi katika miji yenu, ili waweze kusikia na kujifunza kumcha BWANA Mungu wenu na kufuata kwa bidii maneno yote ya sheria hii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kusanya watu wote, wanaume, wanawake, watoto na wageni wanaoishi katika miji yenu, ili waweze kusikia na kujifunza kumcha bwana Mwenyezi Mungu wenu na kufuata kwa bidii maneno yote ya sheria hii.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na kumcha BWANA, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakusanye watu: Wanaume, wanawake, watoto na wageni wanaoishi katika miji yenu, ili kila mmoja asikie maneno haya ya kujifunza kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kuwa waangalifu kutekeleza maneno ya sheria hii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo uwakutanishe watu wote, waume na wake na wana na wageni watakaokuwako malangoni pako, wayasikie, wapate kujifunza, wamwogope Bwana Mungu wenu, wayaangalie na kuyafanya maneno yote ya Maonyo haya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na kumcha BWANA, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutakusanya wanaume, wanawake, watoto na wageni wanaoishi katika miji yenu, kusudi kila mumoja asikie maneno haya ya kujifunza kumwogopa Yawe, Mungu wenu, na kuwa waangalifu kushika maneno ya sheria hii.