Deuteronomy 31:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Mwenyezi-Mungu akamwagiza Yoshua, mwana wa Nuni, akamwambia, “Uwe imara na hodari, maana utawaongoza Waisraeli katika nchi ambayo nimewaapia kuwapa, nami nitakuwa pamoja nawe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akampa Yoshua mwana wa Nuni agizo hili: “Uwe hodari na shujaa, kwa kuwa utawaleta Waisraeli katika nchi niliyowaahidi kwa kiapo, nami mwenyewe nitakuwa pamoja nawe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwagiza Yoshua, mwana wa Nuni, akamwambia, Uwe hodari na moyo mkuu, kwa kuwa utawapeleka wana wa Israeli katika nchi niliyowaapia; nami nitakuwa pamoja nawe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Mwenyezi-Mungu akamwagiza Yoshua, mwana wa Nuni, akamwambia, “Uwe imara na hodari, maana utawaongoza Waisraeli katika nchi ambayo nimewaapia kuwapa, nami nitakuwa pamoja nawe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akampa Yoshua mwana wa Nuni agizo hili: “Uwe hodari na shujaa, kwa kuwa utawaleta Waisraeli katika nchi niliyowaahidi kwa kiapo, nami mwenyewe nitakuwa pamoja nawe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akampa Yoshua mwana wa Nuni agizo hili: “Uwe hodari na shujaa, kwa kuwa utawaleta Waisraeli katika nchi niliyowaahidi kwa kiapo, nami mwenyewe nitakuwa pamoja nawe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwagiza Yoshua, mwana wa Nuni, akamwambia, Uwe hodari na moyo mkuu, kwa kuwa utawapeleka wana wa Israeli katika nchi niliyowaapia; nami nitakuwa pamoja nawe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Mwenyezi-Mungu akamwagiza Yoshua, mwana wa Nuni, akamwambia, “Uwe imara na hodari, maana utawaongoza Waisraeli katika nchi ambayo nimewaapia kuwapa, nami nitakuwa pamoja nawe.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Yosua, mwana wa Nuni, Bwana akamwagiza kwamba: Jipe moyo, upate nguvu! Kwani wewe utawaingiza wana wa Isiraeli katika hiyo nchi, niliyowaapia; nami nitakuwa pamoja na wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwagiza Yoshua, mwana wa Nuni, akamwambia, Uwe hodari na moyo mkuu, kwa kuwa utawapeleka wana wa Israeli katika nchi niliyowaapia; nami nitakuwa pamoja nawe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yawe akamwagiza Yoshua, mwana wa Nuni, akamwambia: “Ukuwe imara na hodari, maana utawaongoza Waisraeli katika inchi ambayo nimewaapia kuwapa, nami nitakuwa pamoja nawe.”