Deuteronomy 31:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana najua mlivyo waasi na wakaidi. Ikiwa mmemwasi Mwenyezi-Mungu wakati niko hai pamoja nanyi, itakuwaje baada ya kifo changu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa ninajua jinsi mlivyo waasi na mlivyo na shingo ngumu. Kama mmekuwa mkiasi dhidi ya Mwenyezi Mungu nikiwa bado niko hai na nikiwa pamoja nanyi, mtaasi mara ngapi baada ya kufa kwangu!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa uasi wako naujua, na shingo yako ngumu; angalieni, mimi nikali hai pamoja nanyi leo, mmekuwa waasi juu ya Bwana; siuze nitakapokwisha kufa!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana najua mlivyo waasi na wakaidi. Ikiwa mmemwasi Mwenyezi-Mungu wakati niko hai pamoja nanyi, itakuwaje baada ya kifo changu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa ninajua jinsi mlivyo waasi na mlivyo na shingo ngumu. Kama mmekuwa mkiasi dhidi ya BWANA nikiwa bado niko hai na nikiwa pamoja nanyi, mtaasi mara ngapi baada ya kufa kwangu!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa ninajua jinsi mlivyo waasi na mlivyo na shingo ngumu. Kama mmekuwa mkiasi dhidi ya bwana nikiwa bado niko hai na nikiwa pamoja nanyi, mtaasi mara ngapi baada ya kufa kwangu!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa uasi wako naujua, na shingo yako ngumu; angalieni, mimi ningali hai pamoja nanyi leo, mmekuwa waasi juu ya BWANA; siuze nitakapokwisha kufa!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana najua mlivyo waasi na wakaidi. Ikiwa mmemwasi Mwenyezi-Mungu wakati niko hai pamoja nanyi, itakuwaje baada ya kifo changu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ninaujua ukatavu wako na ugumu wa ukosi wako; tazameni, siku hizi za leo, ninapokuwa bado mwenye uzima pamoja nanyi, mmekuwa wenye kumkataa Bwana. Tena itakuwaje, nitakapokwisha kufa?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa uasi wako naujua, na shingo yako ngumu; angalieni, mimi nikali hai pamoja nanyi leo, mmekuwa waasi juu ya BWANA; siuze nitakapokwisha kufa!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana ninajua jinsi munavyokuwa waasi na wagumu. Ikiwa mumemwasi Yawe wakati niko muzima pamoja nanyi, itakuwa namna gani nyuma ya kifo changu?