Deuteronomy 31:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawatangulia na kuyaangamiza mataifa yanayoishi huko, ili muimiliki nchi yao. Yoshua atakuwa kiongozi wenu kama alivyosema Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, yeye mwenyewe atavuka mbele yenu. Ataangamiza mataifa haya mbele yenu, nanyi mtaimiliki nchi yao. Pia Yoshua atavuka mbele yenu, kama Mwenyezi Mungu alivyosema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana Mungu wako, ndiye atakayevuka mbele yako, atawaangamiza mataifa haya mbele yako, nawe utawamiliki; na Yoshua atavuka mbele yako, kama Bwana alivyonena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawatangulia na kuyaangamiza mataifa yanayoishi huko, ili muimiliki nchi yao. Yoshua atakuwa kiongozi wenu kama alivyosema Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA Mungu wenu, yeye mwenyewe atavuka mbele yenu. Ataangamiza mataifa haya mbele yenu, nanyi mtaimiliki nchi yao. Pia Yoshua atavuka mbele yenu, kama BWANA alivyosema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana Mwenyezi Mungu wenu, yeye mwenyewe atavuka mbele yenu. Ataangamiza mataifa haya mbele yenu, nanyi mtaimiliki nchi yao. Pia Yoshua atavuka mbele yenu, kama bwana alivyosema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA Mungu wako, ndiye atakayevuka mbele yako, atawaangamiza mataifa haya mbele yako, nawe utawamiliki; na Yoshua atavuka mbele yako, kama BWANA alivyonena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawatangulia na kuyaangamiza mataifa yanayoishi huko, ili muimiliki nchi yao. Yoshua atakuwa kiongozi wenu kama alivyosema Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mungu wako atakutangulia mwenyewe, ukivuka; naye ndiye atakayeyaangamiza mataifa hayo mbele yako, upate kuzichukua nchi zao. Naye Yosua ndiye atakayekuvukisha, kama Bwana alivyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA Mungu wako, ndiye atakayevuka mbele yako, atawaangamiza mataifa haya mbele yako, nawe utawamiliki; na Yoshua atavuka mbele yako, kama BWANA alivyonena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe, Mungu wenu, atawatangulia na kuyaangamiza mataifa yanayoishi huko, kusudi murizi inchi yao. Yoshua atakuwa kiongozi wenu kama vile Yawe alivyosema.