Deuteronomy 31:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Mose akamwita Yoshua, akamwambia mbele ya watu wote wa Israeli, “Uwe Imara na hodari, maana wewe utawaongoza watu hawa kwenda kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu aliwaahidi babu zao; nawe utawakabidhi waimiliki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Musa akamwita Yoshua na akamwambia mbele ya Israeli wote, “Uwe imara na moyo wa ushujaa, kwa kuwa ni lazima uende na watu hawa katika nchi ile Mwenyezi Mungu aliyowaapia baba zao kuwapa, nawe ni lazima uwagawie kama urithi wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akamwita Yoshua, akamwambia machoni pa Israeli wote, Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana utakwenda pamoja na watu hawa hata nchi Bwana aliyowaapia baba zao, ya kwamba atawapa; nawe utawarithisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Mose akamwita Yoshua, akamwambia mbele ya watu wote wa Israeli, “Uwe Imara na hodari, maana wewe utawaongoza watu hawa kwenda kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu aliwaahidi babu zao; nawe utawakabidhi waimiliki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Mose akamwita Yoshua na akamwambia mbele ya Israeli wote, “Uwe imara na moyo wa ushujaa, kwa kuwa ni lazima uende na watu hawa katika nchi ile BWANA aliyowaapia baba zao kuwapa, nawe ni lazima uwagawie kama urithi wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Musa akamwita Yoshua na akamwambia mbele ya Israeli wote, “Uwe imara na moyo wa ushujaa, kwa kuwa ni lazima uende na watu hawa katika nchi ile bwana aliyowaapia baba zao kuwapa, nawe ni lazima uwagawie kama urithi wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akamwita Yoshua, akamwambia machoni pa Israeli wote, Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana utakwenda pamoja na watu hawa hata nchi BWANA aliyowaapia baba zao, ya kwamba atawapa; nawe utawarithisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Mose akamwita Yoshua, akamwambia mbele ya watu wote wa Israeli, “Uwe Imara na hodari, maana wewe utawaongoza watu hawa kwenda kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu aliwaahidi babu zao; nawe utawakabidhi waimiliki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Mose akamwita Yosua, akamwambia machoni pao Waisiraeli wote: Jipe moyo, upate nguvu! Kwani wewe utaingia na watu hawa katika nchi hiyo, Bwana aliyowaapia baba zao kuwapa, kisha utawagawia mafungu yao ya nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akamwita Yoshua, akamwambia machoni pa Israeli wote, Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana utakwenda pamoja na watu hawa hata nchi BWANA aliyowaapia baba zao, ya kwamba atawapa; nawe utawarithisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Musa akamwita Yoshua, akamwambia mbele ya watu wote wa Israeli: “Ukuwe imara na hodari, maana wewe utawaongoza watu hawa kwenda kurizi inchi ambayo Yawe aliwaahidi babu zao, nawe utawapatia wairizi.