Deuteronomy 32:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Israeli walinona na kupiga mateke; walinenepa, wakawa na kitambi na kunawiri; kisha wakamwacha Mungu aliyewaumba, wakamdharau Mwamba wa wokovu wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeshuruni alinenepa na kupiga teke; alikuwa na chakula tele, akawa mzito na akapendeza sana. Akamwacha Mungu aliyemuumba, na kumkataa Mwamba Mwokozi wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Israeli walinona na kupiga mateke; walinenepa, wakawa na kitambi na kunawiri; kisha wakamwacha Mungu aliyewaumba, wakamdharau Mwamba wa wokovu wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeshuruni alinenepa na kupiga teke; alikuwa na chakula tele, akawa mzito na akapendeza sana. Akamwacha Mungu aliyemwumba, na kumkataa Mwamba Mwokozi wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeshuruni alinenepa na kupiga teke; alikuwa na chakula tele, akawa mzito na akapendeza sana. Akamwacha Mungu aliyemuumba, na kumkataa Mwamba Mwokozi wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Israeli walinona na kupiga mateke; walinenepa, wakawa na kitambi na kunawiri; kisha wakamwacha Mungu aliyewaumba, wakamdharau Mwamba wa wokovu wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Yeshuruni* aliponona akapiga mateke kwa kunona na kunenepa na kwa kushiba sana; ndipo, yeye alipomtupa Mungu, naye ndiye aliyemfanya; akambeza yule aliyekuwa mwamba wa wokovu wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa usawa walinona, wakapiga mateke. Walinenepa sana, kisha wakamwacha Mungu aliyewaumba, wakazarau Mulima wa wokovu wao.