Deuteronomy 32:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wamenichochea kuona wivu kwa kitu kisicho mungu, wamenikasirisha kwa sanamu zao. Hivyo nitawafanya waone wivu kwa kisicho watu, nitawakasirisha kwa kutumia taifa la wapumbavu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wamenifanya niwe na wivu kwa kile ambacho si mungu, na kunikasirisha kwa sanamu zao batili. Nitawafanya wawaonee wivu wale ambao si taifa. Nitawafanya wakasirishwe na taifa lile lisilo na ufahamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu; Wamenikasirisha kwa ubatili wao; Nami nitawatia wivu kwa wasio watu, Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wamenichochea kuona wivu kwa kitu kisicho mungu, wamenikasirisha kwa sanamu zao. Hivyo nitawafanya waone wivu kwa kisicho watu, nitawakasirisha kwa kutumia taifa la wapumbavu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wamenifanya niwe na wivu kwa kile ambacho si mungu, na kunikasirisha kwa sanamu zao zisizokuwa na thamani. Nitawafanya wawaonee wivu wale ambao si taifa, nitawafanya wakasirishwe na taifa lile lisilo na ufahamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wamenifanya niwe na wivu kwa kile ambacho si mungu, na kunikasirisha kwa sanamu zao zisizokuwa na thamani. Nitawafanya wawaonee wivu wale ambao si taifa. Nitawafanya wakasirishwe na taifa lile lisilo na ufahamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu; Wamenikasirisha kwa ubatili wao; Nami nitawatia wivu kwa wasio watu, Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wamenichochea kuona wivu kwa kitu kisicho mungu, wamenikasirisha kwa sanamu zao. Hivyo nitawafanya waone wivu kwa kisicho watu, nitawakasirisha kwa kutumia taifa la wapumbavu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wamenichokoza kwa kufuata isiyo miungu, wakanikasirisha kwa kufanya yasiyo na maana, kwa hiyo nami na niwachokoze nikiwaletea watu wasio watu, na niwakasirishe nikiwaletea taifa la watu wasiojua maana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu; Wamenikasirisha kwa ubatili wao; Nami nitawatia wivu kwa wasio watu, Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wamenichochea kuona wivu kwa kitu kisichokuwa mungu, wamenikasirikisha kwa sanamu zao. Hivyo nitawafanya waone wivu juu ya watu wa bure, nitawakasirikisha kwa kutumia taifa la wapumbafu.