Deuteronomy 33:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nchi yake ijae yote yaliyo mema, ibarikiwe kwa wema wa Mwenyezi-Mungu, ambaye alitokea katika kichaka. Baraka hizi ziwashukie watu wa kabila la Yosefu, aliyekuwa mkuu miongoni mwa ndugu zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
pamoja na baraka nzuri mno za ardhi na ukamilifu wake, na upendeleo wake yeye aliyeishi kwenye kichaka kilichokuwa kinawaka moto. Hivi vyote na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, juu ya paji la uso la aliye mkuu miongoni mwa ndugu zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa vitu vilivyo bora vya nchi, na kujaa kwake, Na uradhi wake aliyekaa ndani ya kile kijiti; Na ije baraka juu ya kichwa chake Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliyetengwa na nduguze.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nchi yake ijae yote yaliyo mema, ibarikiwe kwa wema wa Mwenyezi-Mungu, ambaye alitokea katika kichaka. Baraka hizi ziwashukie watu wa kabila la Yosefu, aliyekuwa mkuu miongoni mwa ndugu zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
pamoja na baraka nzuri mno za ardhi na ukamilifu wake, na upendeleo wake yeye aliyeishi kwenye kichaka kilichokuwa kinawaka moto. Hivi vyote na vikae juu ya kichwa cha Yosefu, juu ya paji la uso la aliye mkuu miongoni mwa ndugu zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
pamoja na baraka nzuri mno za ardhi na ukamilifu wake, na upendeleo wake yeye aliyeishi kwenye kichaka kilichokuwa kinawaka moto. Hivi vyote na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, juu ya paji la uso la aliye mkuu miongoni mwa ndugu zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kwa vitu vilivyo bora vya nchi, na kujaa kwake, Na uradhi wake aliyekaa ndani ya kile kichaka; Na ije baraka juu ya kichwa chake Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliyetengwa na nduguze.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nchi yake ijae yote yaliyo mema, ibarikiwe kwa wema wa Mwenyezi-Mungu, ambaye alitokea katika kichaka. Baraka hizi ziwashukie watu wa kabila la Yosefu, aliyekuwa mkuu miongoni mwa ndugu zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo vipaji vizuri vya nchi, navyo vijaavyo ndani yake! Upendeleo wake akaaye porini na ukijie kichwa chake Yosefu, juu ya utosi wake yeye aliyewekwa kwa kutengwa na ndugu zake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa vitu vilivyo bora vya nchi, na kujaa kwake, Na uradhi wake aliyekaa ndani ya kile kijiti; Na ije baraka juu ya kichwa chake Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliyetengwa na nduguze.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Inchi yake ijae yote yanayokuwa mazuri, ibarikiwe kwa huruma wa Yawe, ambaye alitokea katika kichaka. Baraka hizi zishukie watu wa kabila la Yosefu, aliyekuwa mukubwa kati ya wandugu zake.