Deuteronomy 33:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu alikuja kutoka mlima Sinai, alitutokea kutoka mlima Seiri; aliiangaza kutoka mlima Parani. Alitokea kati ya maelfu ya malaika, na moto uwakao katika mkono wake wa kulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alisema: “Mwenyezi Mungu alikuja kutoka Mlima Sinai, akachomoza kama jua juu yao kutoka Mlima Seiri, akaangaza kutoka Mlima Parani. Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu kutoka kusini, kutoka miteremko ya mlima wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu alikuja kutoka mlima Sinai, alitutokea kutoka mlima Seiri; aliiangaza kutoka mlima Parani. Alitokea kati ya maelfu ya malaika, na moto uwakao katika mkono wake wa kulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alisema: “BWANA alikuja kutoka Mlima Sinai, akachomoza kama jua juu yao kutoka Mlima Seiri, akaangaza kutoka Mlima Parani. Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu kutoka kusini, kutoka matelemko ya mlima wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alisema: “ bwana alikuja kutoka Mlima Sinai, akachomoza kama jua juu yao kutoka Mlima Seiri, akaangaza kutoka Mlima Parani. Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu kutoka kusini, kutoka materemko ya mlima wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawajia kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kulia Palikuwa na sheria ya motomoto kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu alikuja kutoka mlima Sinai, alitutokea kutoka mlima Seiri; aliiangaza kutoka mlima Parani. Alitokea kati ya maelfu ya malaika, na moto uwakao katika mkono wake wa kulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akasema: Bwana alitoka Sinai, akakuchelea kama jua toka Seiri, akautokeza mwanga wake toka mlimani kwa Parani, akaja na kutoka katikati yao maelfu kumi ya watakatifu, kuumeni kwake ukawaka moto uliowatokezea Maonyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawaondokea kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe alikuja kutoka mulima Sinai, alitutokea kutoka mulima Seiri, aliangaza kutoka mulima Parani. Alitokea kati ya maelfu ya wamalaika, na moto unaowaka katika mukono wake wa kuume.