Deuteronomy 33:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Heri yenu nyinyi Waisraeli. Nani aliye kama nyinyi, watu mliookolewa na Mwenyezi-Mungu, ambaye ndiye ngao ya msaada wenu, na upanga unaowaletea ushindi! Adui zenu watakuja wananyenyekea mbele yenu, nanyi mtawakanyaga chini.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Israeli, wewe umebarikiwa! Ni nani kama wewe, taifa lililookolewa na Mwenyezi Mungu? Yeye ni ngao yako na msaada wako, na upanga wako uliotukuka. Adui zako watatetemeka mbele yako, nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na Bwana! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Heri yenu nyinyi Waisraeli. Nani aliye kama nyinyi, watu mliookolewa na Mwenyezi-Mungu, ambaye ndiye ngao ya msaada wenu, na upanga unaowaletea ushindi! Adui zenu watakuja wananyenyekea mbele yenu, nanyi mtawakanyaga chini.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee Israeli, wewe umebarikiwa! Ni nani kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA? Yeye ni ngao yako na msaada wako, na upanga wako uliotukuka. Adui zako watatetemeka mbele yako, nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee Israeli, wewe umebarikiwa! Ni nani kama wewe, taifa lililookolewa na bwana? Yeye ni ngao yako na msaada wako, na upanga wako uliotukuka. Adui zako watatetemeka mbele yako, nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Heri yenu nyinyi Waisraeli. Nani aliye kama nyinyi, watu mliookolewa na Mwenyezi-Mungu, ambaye ndiye ngao ya msaada wenu, na upanga unaowaletea ushindi! Adui zenu watakuja wananyenyekea mbele yenu, nanyi mtawakanyaga chini.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenye shangwe ni wewe, Isiraeli! Yuko nani aliyeokolewa na Bwana kama wewe? Yeye ni ngao inayokusaidia, tena ni upanga unaokupatia utukufu. Kwa hiyo adui zako watakunyenyekea, lakini wewe utatembea na kuvikanyaga vilima vyao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Heri yenu ninyi Waisraeli. Nani anayekuwa kama ninyi, watu muliookolewa na Yawe, ambaye ndiye ngao ya musaada wenu, na upanga unaowaletea ushindi! Waadui zenu watakuja wananyenyekea mbele yenu, nanyi mutawakanyaga chini.”