Deuteronomy 4:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mose akaendelea kusema, “Zingatieni basi na kufuata masharti yote na maagizo niliyowafundisha, ili mpate kuishi na kumiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, anawapeni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sikia sasa, ee Israeli, amri na sheria nitakazokufundisha wewe. Zifuate ili upate kuishi na uingie kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zako, anawapa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu niwafundishazo, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi awapayo Bwana, Mungu wa baba zenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mose akaendelea kusema, “Zingatieni basi na kufuata masharti yote na maagizo niliyowafundisha, ili mpate kuishi na kumiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, anawapeni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sikia sasa, Ee Israeli, amri na sheria nitakazokufundisha wewe. Zifuate ili upate kuishi na uingie kuimiliki nchi ambayo BWANA, Mungu wa baba zako anawapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sikia sasa, ee Israeli, amri na sheria nitakazokufundisha wewe. Zifuate ili upate kuishi na uingie kuimiliki nchi ambayo bwana, Mungu wa baba zako anawapa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu ninazowafundisha, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi anayowapa BWANA, Mungu wa baba zenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mose akaendelea kusema, “Zingatieni basi na kufuata masharti yote na maagizo niliyowafundisha, ili mpate kuishi na kumiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, anawapeni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa Isiraeli, yasikilize maongozi na maamuzi, nitakayowafundisha, myafanye, mpate kupona na kuiingia na kuichukua hiyo nchi, Bwana Mungu wa baba zenu atakayowapa, iwe yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu niwafundishazo, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wa baba zenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa akaendelea kusema: “Mushike basi na kufuata masharti na maagizo niliyowafundisha, kusudi mupate kuishi na kurizi inchi ambayo Yawe, Mungu wa babu zenu, anawapa.