Deuteronomy 4:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Mwenyezi-Mungu aliongea nanyi kutoka katikati ya moto huo; mliyasikia maneno aliyosema lakini hamkumwona; mlisikia tu sauti yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mwenyezi Mungu alipozungumza nanyi kutoka kati ya moto. Mkasikia sauti ya maneno lakini hamkuona umbo, kulikuwa na sauti tu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akasema nanyi kutoka kati ya moto; mkasikia sauti ya maneno, lakini hamkuona umbo lo lote; sauti tu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Mwenyezi-Mungu aliongea nanyi kutoka katikati ya moto huo; mliyasikia maneno aliyosema lakini hamkumwona; mlisikia tu sauti yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo BWANA alipozungumza nanyi kutoka katika moto. Mkasikia sauti ya maneno lakini hamkuona umbo, kulikuwa na sauti tu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo bwana alipozungumza nanyi kutoka moto. Mkasikia sauti ya maneno lakini hamkuona umbo, kulikuwa na sauti tu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akasema nanyi kutoka kati ya moto; mkasikia sauti ya maneno, lakini hamkuona umbo lolote; sauti tu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Mwenyezi-Mungu aliongea nanyi kutoka katikati ya moto huo; mliyasikia maneno aliyosema lakini hamkumwona; mlisikia tu sauti yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana aliposema nanyi toka motoni, nanyi mkazisikia sauti za maneno yake, lakini hakuna mwenye mwili, mliyemwona, ni kuzisikia hizo sauti tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akasema nanyi kutoka kati ya moto; mkasikia sauti ya maneno, lakini hamkuona umbo lo lote; sauti tu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yawe akasema nanyi kutoka katikati ya moto huo. Mukasikia maneno aliyosema lakini hamukumwona. Mulisikia tu sauti yake.