Deuteronomy 4:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo Mwenyezi-Mungu aliniamuru niwafundishe masharti na maagizo yote ambayo mnapaswa kuyatekeleza katika nchi mnayokwenda kuimiliki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Mwenyezi Mungu alinielekeza wakati huo kuwafundisha ninyi sheria na amri ambazo mnapaswa kuzifuata katika nchi ambayo mnavuka Yordani kuimiliki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akaniamuru wakati ule niwafundishe maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo Mwenyezi-Mungu aliniamuru niwafundishe masharti na maagizo yote ambayo mnapaswa kuyatekeleza katika nchi mnayokwenda kuimiliki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye BWANA alinielekeza wakati huo kuwafundisha ninyi sheria na amri ambazo mnapaswa kuzifuata katika nchi ambayo mnavuka Yordani kuimiliki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye bwana alinielekeza wakati huo kuwafundisha ninyi sheria na amri ambazo mnapaswa kuzifuata katika nchi ambayo mnavuka Yordani kuimiliki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akaniamuru wakati ule niwafundishe maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo Mwenyezi-Mungu aliniamuru niwafundishe masharti na maagizo yote ambayo mnapaswa kuyatekeleza katika nchi mnayokwenda kuimiliki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi nami Bwana akaniagiza siku hizo kuwafundisha maongozi na maamuzi, myafanye katika hiyo nchi, mnayotaka kuivukia, mwichukue, iwe yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akaniamuru wakati ule niwafundishe maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo Yawe akaniamuru niwafundishe masharti na maagizo yote ambayo munapaswa kutimiza katika inchi munayokwenda kuirizi.