Deuteronomy 4:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa hiyo muwe waangalifu msije kusahau kwamba: Mwenyezi-Mungu alipoongea nanyi kule mlimani Horebu katikati ya moto hamkumwona kwa umbo. Kwa sababu hiyo jihadharini sana,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hamkuona umbo la aina yoyote siku ambayo Mwenyezi Mungu alizungumza nanyi kule Horebu kutoka kati ya moto. Kwa hiyo mjihadhari kwa uangalifu sana,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yo yote siku ile Bwana aliyosema nanyi kutoka kati ya moto;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa hiyo muwe waangalifu msije kusahau kwamba: Mwenyezi-Mungu alipoongea nanyi kule mlimani Horebu katikati ya moto hamkumwona kwa umbo. Kwa sababu hiyo jihadharini sana,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hamkuona umbo la aina yo yote siku ambayo BWANA alizungumza na ninyi kule Horebu kutoka kwenye moto. Kwa hiyo mjihadhari kwa uangalifu sana,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hamkuona umbo la aina yoyote siku ambayo bwana alizungumza nanyi kule Horebu kutoka kwenye moto. Kwa hiyo mjihadhari kwa uangalifu sana,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yoyote siku ile BWANA aliyosema nanyi kutoka kati ya moto;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa hiyo muwe waangalifu msije kusahau kwamba: Mwenyezi-Mungu alipoongea nanyi kule mlimani Horebu katikati ya moto hamkumwona kwa umbo. Kwa sababu hiyo jihadharini sana,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ziangalieni sana roho zenu! Kwani hamkuona mwenye mwili ye yote siku hiyo, Bwana aliposema nanyi kule Horebu toka motoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yo yote siku ile BWANA aliyosema nanyi kutoka kati ya moto;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kwa hiyo mukuwe waangalifu kusudi musisahau kwamba Yawe aliposema nanyi kule kwenye milima ya Horebu katikati ya moto hamukumwona kwa umbo. Kwa sababu hiyo mufanye angalisho sana,