Deuteronomy 4:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jihadharini ili wakati mtakapoangalia na kutazama jua, mwezi na nyota na jeshi lote la mbinguni, msije mkashawishiwa kuviabudu na kuvitumikia, maana vitu hivyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliviumba kwa ajili ya watu wote duniani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Na utazamapo juu angani na ukaliona jua, mwezi na nyota na vyote vinavyoipamba mbingu, usije ukashawishiwa kuviinamia na kuviabudu vitu ambavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alivigawia mataifa yote chini ya mbingu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jihadharini ili wakati mtakapoangalia na kutazama jua, mwezi na nyota na jeshi lote la mbinguni, msije mkashawishiwa kuviabudu na kuvitumikia, maana vitu hivyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliviumba kwa ajili ya watu wote duniani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Na utazamapo juu angani na ukaliona jua, mwezi na nyota na vyote vinavyoipamba mbingu, usije ukashawishiwa kuviinamia na kuviabudu vile ambavyo BWANA Mungu wenu alivyogawia mataifa yote chini ya mbingu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Na utazamapo juu angani na ukaliona jua, mwezi na nyota na vyote vinavyoipamba mbingu, usije ukashawishiwa kuviinamia na kuviabudu vile ambavyo bwana Mwenyezi Mungu wenu alivyogawia mataifa yote chini ya mbingu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo BWANA, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jihadharini ili wakati mtakapoangalia na kutazama jua, mwezi na nyota na jeshi lote la mbinguni, msije mkashawishiwa kuviabudu na kuvitumikia, maana vitu hivyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliviumba kwa ajili ya watu wote duniani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wala usiyainue macho yako na kuyaelekeza mbinguni, ulitazame jua na mwezi na nyota, hivyo vikosi vya mbinguni, usijaribiwe kuviangukia na kuvitumikia, kwa kuwa Bwana Mungu wako aliviwekea makabila yote pia yaliyoko chini ya mbingu yote nzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo BWANA, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufanye angalisho kusudi wakati mutakapoangalia na kuona nyota, vitu vyote vya mbinguni, musivutwe kuviabudu na kuvitumikia. Vitu hivyo Yawe amewaachia watu wengine waviabudu.