Deuteronomy 4:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini nyinyi ndio watu aliowakomboa kutoka Misri katika tanuri la chuma. Aliwatoeni huko ili muwe watu wake kama vile mlivyo hivi leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ninyi, Mwenyezi Mungu amewatoa kutoka tanuru la kuyeyushia chuma, kutoka Misri, kuwa watu wa urithi wake, kama mlivyo sasa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali Bwana amewatwaa ninyi, na kuwatoa katika tanuu ya chuma, katika Misri, mpate kuwa watu wa urithi kwake, kama mlivyo leo hivi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini nyinyi ndio watu aliowakomboa kutoka Misri katika tanuri la chuma. Aliwatoeni huko ili muwe watu wake kama vile mlivyo hivi leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kwenu ninyi, BWANA amewatoa kutoka kwenye tanuru ya kuyeyushia chuma, katika Misri kuwa watu wa urithi wake kama mlivyo sasa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kwenu ninyi, bwana amewatoa kutoka kwenye tanuru ya kuyeyushia chuma, katika Misri kuwa watu wa urithi wake kama mlivyo sasa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali BWANA amewatwaa ninyi, na kuwatoa katika tanuri ya chuma, katika Misri, mpate kuwa watu wa urithi kwake, kama mlivyo hivi leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini nyinyi ndio watu aliowakomboa kutoka Misri katika tanuri la chuma. Aliwatoeni huko ili muwe watu wake kama vile mlivyo hivi leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ninyi Bwana aliwachukua na kuwatoa katika tanuru ya kuyeyushia vyuma, ndio Misri, mwe kabila llilo lake yeye mwenyewe, kama inavyoelekea leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali BWANA amewatwaa ninyi, na kuwatoa katika tanuu ya chuma, katika Misri, mpate kuwa watu wa urithi kwake, kama mlivyo leo hivi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninyi ndio watu aliowakomboa kutoka Misri katika furu la chuma. Aliwatoa huko kusudi mukuwe watu wake kama vile munavyokuwa hivi leo.