Deuteronomy 4:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jihadharini sana msije mkasahau agano ambalo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amefanya nanyi; msijifanyie sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu chochote ambacho Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amewakataza kumfananisha,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jihadharini msilisahau agano la Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, lile alilofanya nanyi; msijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote ambacho Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewakataza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la Bwana, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu cho chote ulichokatazwa na Bwana, Mungu wenu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jihadharini sana msije mkasahau agano ambalo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amefanya nanyi; msijifanyie sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu chochote ambacho Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amewakataza kumfananisha,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jihadharini msilisahau Agano la BWANA Mungu wenu lile alilofanya nanyi; msijitengenezee sanamu katika umbo la kitu cho chote ambacho BWANA Mungu wenu amewakataza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jihadharini msilisahau Agano la bwana Mwenyezi Mungu wenu lile alilofanya nanyi; msijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote ambacho bwana Mwenyezi Mungu wenu amewakataza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la BWANA, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu chochote ulichokatazwa na BWANA, Mungu wenu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jihadharini sana msije mkasahau agano ambalo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amefanya nanyi; msijifanyie sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu chochote ambacho Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amewakataza kumfananisha,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jiangalieni, msilisahau Agano la Bwana Mungu wenu, alilolifanya nanyi, msijifanyizie kinyago cho chote cha kuchongwa, wala cha kuyeyushwa kwa mfano wo wote, Bwana Mungu wako aliokukataza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la BWANA, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu cho chote ulichokatazwa na BWANA, Mungu wenu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufanye angalisho sana kusudi musisahau agano ambalo Yawe, Mungu wenu, amefanya nanyi. Musijifanyie sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu chochote ambacho Yawe, Mungu wenu, amewakataza kumufananisha nacho,