Deuteronomy 4:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtakapokuwa mmekaa katika nchi hiyo, mkapata watoto na wajukuu na kuwa wazee, kama mkianza kupotoka na kujifanyia sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu chochote, mkafanya uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kumkasirisha,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya kuwa na watoto na wajukuu na kuishi katika nchi hiyo siku nyingi, tena mkijichafua na kutengeneza sanamu ya aina yoyote, mkifanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kumfanya awe na hasira,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Utakapozaa wana, na wana wa wana, mkisha kuwa katika nchi siku nyingi, mkajiharibu na kufanya sanamu ya kuchonga kwa umbo la kitu cho chote, mkafanya ambayo ni maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, na kumtia hasira;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mtakapokuwa mmekaa katika nchi hiyo, mkapata watoto na wajukuu na kuwa wazee, kama mkianza kupotoka na kujifanyia sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu chochote, mkafanya uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kumkasirisha,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kuwa na watoto na wajukuu na kuishi katika nchi hiyo siku nyingi, tena kama mkijichafua na kutengeneza sanamu ya aina yo yote, mkifanya maovu machoni pa BWANA Mungu wenu na kumfanya awe na hasira,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kuwa na watoto na wajukuu na kuishi katika nchi hiyo siku nyingi, tena kama mkijichafua na kutengeneza sanamu ya aina yoyote, mkifanya maovu machoni pa bwana Mwenyezi Mungu wenu na kumfanya awe na hasira,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Utakapozaa wana, na wana wa wanao, mkisha kuwa katika nchi siku nyingi, mkajiharibu na kufanya sanamu ya kuchonga kwa umbo la kitu chochote, mkafanya ambayo ni maovu machoni pa BWANA Mungu wako, na kumtia hasira;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtakapokuwa mmekaa katika nchi hiyo, mkapata watoto na wajukuu na kuwa wazee, kama mkianza kupotoka na kujifanyia sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu chochote, mkafanya uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kumkasirisha,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtakapozaa wana na wana wa wana, mwe wazee katika nchi hiyo, msijiponze na kujifanyizia kinyago cho chote cha kuchongwa, wala cha kuyeyushwa, kwani hivyo mtafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana Mungu wenu, mmkasirishe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Utakapozaa wana, na wana wa wana, mkisha kuwa katika nchi siku nyingi, mkajiharibu na kufanya sanamu ya kuchonga kwa umbo la kitu cho chote, mkafanya ambayo ni maovu machoni pa BWANA, Mungu wako, na kumtia hasira;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mimi leo ninaita mbingu na dunia zishuhudie juu yenu. Mutakapokuwa mukikaa katika inchi hiyo, mukipata watoto na wajukuu na kuwa wazee, kama mukianza kupotoka na kujifanyia sanamu katika umbo la kitu chochote, mukifanya uovu mbele ya Yawe, Mungu wenu, na kumukasirikisha, mara moja mutaangamia kabisa katika inchi ambayo munaenda kurizi huko ngambo ya muto Yordani. Hamutaishi huko muda murefu, lakini mutaangamizwa kabisa.