Deuteronomy 4:26 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
basi, mimi leo naziita mbingu na dunia zishuhudie kati yenu; nawaambieni kwamba mara moja mtaangamia kabisa katika nchi ambayo mnaenda kuimiliki huko ngambo ya mto Yordani. Hamtaishi huko muda mrefu, bali mtaangamizwa kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yenu siku hii kwamba mtaangamia mara moja kutoka katika nchi ile ambayo mnavuka Yordani kuimiliki. Hamtaishi kule kwa muda mrefu bali kwa hakika mtaangamizwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nawashuhudizia mbingu na nchi hivi leo, kwamba karibu mtaangamia kabisa juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki, hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake, ila mtaangamizwa kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
basi, mimi leo naziita mbingu na dunia zishuhudie kati yenu; nawaambieni kwamba mara moja mtaangamia kabisa katika nchi ambayo mnaenda kuimiliki huko ng'ambo ya mto Yordani. Hamtaishi huko muda mrefu, bali mtaangamizwa kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yenu siku hii kwamba mtaangamia mara moja kutoka katika nchi ile ambayo mnavuka Yordani kuimiliki. Hamtaishi kule kwa muda mrefu bali kwa hakika mtaangamizwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yenu siku hii kwamba mtaangamia mara moja kutoka nchi ile ambayo mnavuka Yordani kuimiliki. Hamtaishi kule kwa muda mrefu bali kwa hakika mtaangamizwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naziita mbingu na nchi hivi leo kushuhudia, kwamba karibu mtaangamia kabisa juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki, hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake, ila mtaangamizwa kabisa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
basi, mimi leo naziita mbingu na dunia zishuhudie kati yenu; nawaambieni kwamba mara moja mtaangamia kabisa katika nchi ambayo mnaenda kuimiliki huko ngambo ya mto Yordani. Hamtaishi huko muda mrefu, bali mtaangamizwa kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo nazitaja mbingu na nchi, ziwashuhudie leo hivi, ya kama hivyo mtaangamia upesi na kutoweka katika nchi hiyo, mnayovukia Yordani, mje kuichukua, iwe yenu, hamtakaa siku nyingi ndani yake, ila mtaangamizwa kabisa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nawashuhudizia mbingu na nchi hivi leo, kwamba karibu mtaangamia kabisa juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki, hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake, ila mtaangamizwa kabisa.