Deuteronomy 4:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, watu walikwisha sikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama nyinyi mlivyosikia, wakabaki hai?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, kuna watu wengine wowote waliosikia sauti ya Mungu ikizungumza kwenye moto, kama mlivyosikia, nao wakaishi?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Watu wakati wo wote wameisikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama wewe ulivyosikia, wasife?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, watu walikwisha sikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama nyinyi mlivyosikia, wakabaki hai?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, kuna watu wengine wo wote waliosikia sauti ya Mungu ikizungumza kwenye moto, kama mlivyosikia, nao wakaishi?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, kuna watu wengine wowote waliosikia sauti ya Mungu ikizungumza kwenye moto, kama mlivyosikia, nao wakaishi?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Kuna wakati wowote watu wameisikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama wewe ulivyosikia, na wakaendelea kuishi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, watu walikwisha sikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama nyinyi mlivyosikia, wakabaki hai?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wako watu walioisikia sauti ya Mungu, akisema toka motoni, kama wewe ulivyoisikia, kisha wawepo wenye uzima?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Watu wakati wo wote wameisikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama wewe ulivyosikia, wasife?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu walikwisha kusikia sauti ya Mungu ikisema toka katikati ya moto, kama ninyi mulivyosikia, wakabaki wazima?