Deuteronomy 4:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, kuna Mungu yeyote mwingine aliyejaribu kamwe kwenda kujichukulia taifa lake kutoka taifa jingine, kama vile Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alivyofanya, kwa kutumia majaribio, ishara na maajabu, kwa vita na kwa nguvu yake kuu, akasababisha mambo ya kutisha ambayo nyinyi mlishuhudia kwa macho yenu kule Misri?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, kuna mungu yeyote amepata kujaribu mwenyewe kuchukua taifa moja kutoka taifa lingine, kwa mapigo, kwa ishara za miujiza na maajabu, kwa vita, kwa mkono wenye nguvu na mkono ulionyooshwa au kwa matendo makuu ya kutisha, kama yale ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, aliyofanya kwa ajili yenu huko Misri mbele ya macho yenu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa toka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, na kwa ishara, na kwa maajabu, na kwa vita, na kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa maogofya makuu, kama vile Bwana, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, kuna Mungu yeyote mwingine aliyejaribu kamwe kwenda kujichukulia taifa lake kutoka taifa jingine, kama vile Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alivyofanya, kwa kutumia majaribio, ishara na maajabu, kwa vita na kwa nguvu yake kuu, akasababisha mambo ya kutisha ambayo nyinyi mlishuhudia kwa macho yenu kule Misri?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, kuna mungu ye yote amepata kujaribu mwenyewe kuchukua taifa moja kutoka taifa lingine, kwa mapigo, kwa ishara za miujiza na maajabu, kwa vita, kwa mkono wenye nguvu na mkono ulionyooshwa au kwa matendo makuu yakutisha, kama yale ambayo BWANA Mungu wenu aliyofanya kwa ajili yenu huko Misri mbele ya macho yenu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, kuna mungu yeyote amepata kujaribu mwenyewe kuchukua taifa moja kutoka taifa lingine, kwa mapigo, kwa ishara za miujiza na maajabu, kwa vita, kwa mkono wenye nguvu na mkono ulionyooshwa au kwa matendo makuu ya kutisha, kama yale ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu aliyofanya kwa ajili yenu huko Misri mbele ya macho yenu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa kutoka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, ishara, maajabu, vita, mkono hodari, mkono ulionyoshwa, na vitisho vikuu, kama vile BWANA, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, kuna Mungu yeyote mwingine aliyejaribu kamwe kwenda kujichukulia taifa lake kutoka taifa jingine, kama vile Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alivyofanya, kwa kutumia majaribio, ishara na maajabu, kwa vita na kwa nguvu yake kuu, akasababisha mambo ya kutisha ambayo nyinyi mlishuhudia kwa macho yenu kule Misri?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Au Mungu alijaribu hata penginepo kuja kujichukulia taifa moja katikati ya mataifa mengine kwa majaribu na kwa vielekezo na kwa vioja na kwa kupiga vita na kwa kutoa nguvu za kiganja chake na kwa kuukunjua mkono wake na kwa matisho makuu yanayoogopesha, kama Bwana Mungu wenu alivyowafanyizia ninyi kule Misri machoni pako?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa toka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, na kwa ishara, na kwa maajabu, na kwa vita, na kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa maogofya makuu, kama vile BWANA, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuna Mungu yeyote mwingine aliyejaribu hata kidogo kwenda kujitwalia taifa lake kutoka taifa lingine, kama vile Yawe, Mungu wenu, alivyofanya, kwa kutumia majaribio, vitambulisho, maajabu, vita, na vitisho? Hapana. Lakini mulishuhudia kwa macho yenu namna Yawe alivyofanya kwa mukono wake wenye nguvu kabisa kule Misri.