Deuteronomy 4:36 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliwafanya muisikie sauti yake kutoka mbinguni ili aweze kuwafunza nidhamu; na hapa duniani akawafanya mwone moto wake mkubwa na kusikia maneno yake kutoka katikati ya moto huo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka mbinguni amewasikizisha sauti yake ili kuwaadilisha. Hapa duniani aliwaonesha moto wake mkubwa, nanyi mlisikia maneno yake kutoka kati ya ule moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kutoka mbinguni amekusikizisha sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonyesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake toka kati ya moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliwafanya muisikie sauti yake kutoka mbinguni ili aweze kuwafunza nidhamu; na hapa duniani akawafanya mwone moto wake mkubwa na kusikia maneno yake kutoka katikati ya moto huo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka mbinguni amewasikizisha sauti yake ili kuwaadilisha. Hapa duniani aliwaonyesha moto wake mkubwa, nanyi mlisikia maneno yake kutoka kwenye ule moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka mbinguni amewasikizisha sauti yake ili kuwaadilisha. Hapa duniani aliwaonyesha moto wake mkubwa, nanyi mlisikia maneno yake kutoka kwenye ule moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kutoka mbinguni amekufanya usikie sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake kutoka katika moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliwafanya muisikie sauti yake kutoka mbinguni ili aweze kuwafunza nidhamu; na hapa duniani akawafanya mwone moto wake mkubwa na kusikia maneno yake kutoka katikati ya moto huo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uliisikia sauti yake, ikitoka mbinguni, ipate kukuonya, nako huku nchini alikuonyesha moto wake mkubwa, nako kutoka humo motoni ukaisikia sauti yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kutoka mbinguni amekusikizisha sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonyesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake toka kati ya moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliwafanya muisikie sauti yake kutoka mbinguni kusudi aweze kuwafundisha; na hapa katika dunia akawafanya muone moto wake mukubwa na kusikia maneno yake kutoka katikati ya moto huo.