Deuteronomy 4:42 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
ambamo mtu ataweza kukimbilia na kujisalimisha, kama ameua mtu ambaye si adui yake kwa bahati mbaya. Mtu kama huyo ataweza kukimbilia katika mji mmojawapo na kuyaokoa maisha yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ambayo mtu yeyote aliyemuua mtu angeweza kukimbilia ikiwa amemuua jirani yake bila kukusudia na bila kuwa na chuki naye siku zilizopita. Angeweza kukimbilia katika mmoja ya miji hii na kuokoa maisha yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ili kwamba amwuaye mtu apate kukimbilia huko, amwuaye jirani yake pasipo kujua, wala hakumchukia tangu hapo; ili apate kuishi akimbiliapo mmojawapo miji hiyo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
ambamo mtu ataweza kukimbilia na kujisalimisha, kama ameua mtu ambaye si adui yake kwa bahati mbaya. Mtu kama huyo ataweza kukimbilia katika mji mmojawapo na kuyaokoa maisha yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ambayo mtu ye yote aliyemwua mtu angeweza kukimbilia ikiwa amemwua jirani yake bila kukusudia na bila kuwa na chuki naye siku zilizopita. Angeweza kukimbilia katika mmojawapo ya miji hii na kuokoa maisha yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ambayo mtu yeyote aliyemuua mtu angeweza kukimbilia ikiwa amemuua jirani yake bila kukusudia na bila kuwa na chuki naye siku zilizopita. Angeweza kukimbilia katika mmojawapo ya miji hii na kuokoa maisha yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili kwamba amwuaye mtu apate kukimbilia huko, amwuaye jirani yake pasipo kujua, wala hakumchukia tangu hapo; ili apate kuishi akimbiliapo katika mmojawapo wa miji hiyo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
ambamo mtu ataweza kukimbilia na kujisalimisha, kama ameua mtu ambaye si adui yake kwa bahati mbaya. Mtu kama huyo ataweza kukimbilia katika mji mmojawapo na kuyaokoa maisha yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mtu apate kuikimbilia, kama amemwua mwenziwe pasipo kujua, naye alipokuwa si mchukivu wake tangu zamani, basi, atakapokimbilia mmojawapo hiyo miji, awe amepona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ili kwamba amwuaye mtu apate kukimbilia huko, amwuaye jirani yake pasipo kujua, wala hakumchukia tangu hapo; ili apate kuishi akimbiliapo mmojawapo miji hiyo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
ambamo mutu ataweza kukimbilia na kujiponyesha, kama ameua mutu ambaye si adui yake kwa bahati mbaya. Mutu kama huyo ataweza kukimbilia katika muji mumoja na kuyaokoa maisha yake.