Deuteronomy 4:46 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wakiwa ngambo ya mto Yordani, katika bonde lililo mbele ya Beth-peori, katika nchi iliyokuwa ya mfalme Sihoni wa Waamori, aliyetawala kutoka mjini Heshboni, ambaye Mose na Waisraeli walimshinda walipotoka Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nao walikuwa katika bonde karibu na Beth-Peori mashariki mwa Yordani, katika nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala Heshboni; naye alishindwa na Musa na Waisraeli walipotoka Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ng'ambo ya Yordani, katika bonde lililoelekea Beth-peori, katika nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni ndiye aliyepigwa na Musa na wana wa Israeli, walipotoka Misri;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wakiwa ng'ambo ya mto Yordani, katika bonde lililo mbele ya Beth-peori, katika nchi iliyokuwa ya mfalme Sihoni wa Waamori, aliyetawala kutoka mjini Heshboni, ambaye Mose na Waisraeli walimshinda walipotoka Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nao walikuwa katika bonde karibu na Beth-Peori mashariki ya Yordani, katika nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala Heshboni, naye alishindwa na Mose na Waisraeli walipokuja toka Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nao walikuwa katika bonde karibu na Beth-Peori mashariki ya Yordani, katika nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala Heshboni, naye alishindwa na Musa na Waisraeli walipokuja toka Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ng'ambo ya Yordani, katika bonde lililoelekea Beth-peori, katika nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni ndiye aliyepigwa na Musa na wana wa Israeli, walipotoka Misri;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wakiwa ngambo ya mto Yordani, katika bonde lililo mbele ya Beth-peori, katika nchi iliyokuwa ya mfalme Sihoni wa Waamori, aliyetawala kutoka mjini Heshboni, ambaye Mose na Waisraeli walimshinda walipotoka Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aliyasema ng'ambo ya huku ya Yordani katika bonde linaloelekea Beti-Peori katika nchi ya Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekaa Hesiboni, Mose na wana wa Isiraeli waliyempiga walipotoka Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ng’ambo ya Yordani, katika bonde lililoelekea Beth-peori, katika nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni ndiye aliyepigwa na Musa na wana wa Israeli, walipotoka Misri;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wakiwa ngambo ya muto Yordani, katika bonde linalokuwa mbele ya Beti-Peori, katika inchi iliyokuwa ya mufalme Sihoni wa Waamori, aliyetawala kutoka katika muji wa Hesiboni, ambaye Musa na Waisraeli walimushinda walipotoka Misri.